HATIMAYE IDRIS AKATA KIU YA WATANZANI BIG BROTHER AFRICA


 Ikiwa ni siku ya 63 tangu kuanza kwa mashindano ya "Big Brother Africa" na ndiyo siku ambayo imefanyika fainali ya shindano hilo kwa mwaka huu 2014.

Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa ni baada ya usiku huu wa Disemba 7 Tanzania kuweka historia nyingine ambapo mwakilishi aliyekuwa anaiwakilisha Tanzania Idris Sultan amefanikiwa kuibuka mshindi katika shindano hilo.

Idris Sultan mshindi wa Big Brother Africa 2014
 Aidha, itakumbukwa kwamba kwamba, Tanzania ndiyo nchi pekee iliyokuwa imebakiwa na mshiriki wake ndani ya Jumba la BBA katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku tukishuhudia namna ambavyo mastaa wengi wakitoa ushirikiano mkubwa kwa mshiriki huyo na hatimaye sasa kaibuka mshindi.
ambaye ni Idris.

Idris Sultan pia ni mpiga picha na graphic designer anayefanya kazi kwenye kampuni ya I-View Studios, na kutokana na ushindi wake huo atapata kiasi cha shilingi milioni 514.

Ni haki yako kupata habari muda wote inapotokea kupitia habarimkusanyiko.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname