Bara la Afrika ndio bara pekee duniani liloweza kubarikiwa kuwa na wanyama wa tano wakubwa wa porini.
Wanyama hawa hawakuchanguliwa kwakuangalia ukubwa wa miili yao ila nikutokana ugumu wa kuwindwa na pia ndio wanyama hatari na wenye hasira kali kuliko wote. Wanyama hao ni pamoja na Tembo, Faru, Nyati , Simba na Chui.
Nchi pekee barani Afrika ambazo wanyama hawa wakubwa wa tano hupatikana ni pamoja na nchi ya Tanzania, Botswana, Zambia, Uganda, Namibia, Ethiopia, Afrika ya Kusini, Kenya, Zimbambwe, Kongo, na Malawi.
Tembo
Faru
Faru ni mamalia wa pili kwa ukubwa baada ya tembo, huku kukiwa na spishi mbili za faru wapatikanao barani Afrika ambazo ni faru mweupe na faru mweusi. Utofauti ya faru hawa ni kwenye namna ya midomo yao ilivyo kaa na sio rangi kama wengi wananyodhani.
Kwa bahati mbaya hivi sasa wanyama hao wamekuwa wakipungua kutokana na ongezeko la ujangili uliokithiri barani Afrika. Pembe ya faru inasadikika kutumika kama tiba ya magongwa mbalimbali hasa bara la Asia.
Mwaka 2012 pembe ya faru ilikuwa ikiuzwa dola 60,000 kwa kilo. Tukiweza kuzuia ujangili faru wataweza kuishi hadi miaka 30-50.
Nyati
Nyati dume hukuwa na kufika futi 4-6 na kilo 700, nyati amehesabika kupoteza maisha ya watu wengi kuzidi wanyama wengine wa porini. Ni mnyama mwenye hasira kali sana na pia ni hatari sana.
Mnyama huyu humuwia vigumu hata samba wakati wa kuwinda na humbidi samba kupata msaada kutoka kwa wenzake ndio waweze kumuangusha nyati mmoja.
Simba
Simba ndio paka mkumbwa kati ya wapatikano bara la Afrika. Dume huwa na manyoya kuanzia kwenye mabega yake nakuelekea kwenye kichwa chake. Simba huweza kuishi hadi miaka kumi na nane akiwa porini, lakini wengi wao hupoteza maisha kutokana na kupingana kati ya wenyewe kwa wenyewe.
Simba jike ataishi kwenye familia yake huku dume atatolewa katika familia akiwa na miaka 2-4 na kuanza kwenda kujitengemea.
Chui
Ni moja kati ya paka wakubwa watano wapatikanao porini ila imekuwa vigumu sana kumuona chui hata ukiwa porini nikutokana na mazingira ambayo amekuwa akishi. Chui upendelea kuishi juu ya miti na kutumia mazingira hayo kama njia yake ya kujilinda.
Chui ni nusu ya uzito wa simba ila anauwezo wa kubeba mnyama na kupanda nae juu ya mti.
ZUIA UJANGILI KULINDA VIUMBE VINAVYO KARIBIA KUPOTEA
Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel kutoka kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's Ltd, ambao ni mabingwa wa kuandaa safari za kitalii pamoja na kukodisha magari kwa gharama nafuu sana, endapo ungependa kujaribu huduma zao hebu watafute kwa simu namba 0654 022 054 / 0715 437 283 au kupitia www.samscarental.com.
imekaa vizuri japo hmjawa
ReplyDeletechambua wanyama kwa undani zaidi
Habari Mkusanyiko: Fahamu Undani Wa Wanyama Wakubwa Watano Porini >>>>> Download Now
ReplyDelete>>>>> Download Full
Habari Mkusanyiko: Fahamu Undani Wa Wanyama Wakubwa Watano Porini >>>>> Download LINK
>>>>> Download Now
Habari Mkusanyiko: Fahamu Undani Wa Wanyama Wakubwa Watano Porini >>>>> Download Full
>>>>> Download LINK