HIVI UNAFAHAMU KUWA MNYAMA KIBOKO HUTOA JASHO LINALOFANANA NA DAMU? TAFADHALI TWENDE SAMBAMBA HAPA KATIKA JICHO LETU PORINI



Habari za leo msomaji wetu wa habarimkusanyiko.blogspot.com, karibu sana katika “Jicho Letu Porini” inayokujia kwa wiki mara moja kupitia blog hii, na leo tutakwenda kuangalia kuhusiana na Kiboko (Hippopotamus amphibius).

Kiboko ni mamalia mkubwa wa familia ya Hippopotamidae. Huku akiwa anashindana na kifaru juu ya cheo cha kuwa mnyama mzito wa pili kwenye nchi kavu baada ya Tembo..

Hippopotamus ni neno lenye maana ya Kiboko kwa Kiswahili na asili ya neno hilo ni Ugiriki likiwa na maana ya ‘Hippo’ ni 'mto' na ‘Potamus’ ni 'farasi' nakufanya kiboko kujulikana kwa jina la utani kama 'farasi wa mtoni'.

Kiboko ni miongoni mwa mnyama mkubwa na mwenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu, huku ujazo-nene wa mnyama huyu ukimruhusu kuzama na kuogelea chini kabisa mwa mto.

Kiboko nao huchukuliwa kama mnyama mkubwa, lakini tofauti na wanyama wengine wakubwa, kiboko huishi kwenye maji baridi ya mito na maziwa. Kutokana na umbo lao kubwa, ni vigumu kupima uzito wao wakiwa mwituni, lakini hata hivyo makadilio mengi ya uzito yanatokana na operesheni za kuwapunguza zilizofanyika mnamo mwaka 1960.

Aidha, wastani wa uzito wa kiboko dume inaelezwa kuwa ni kg 1500 - 1800. Huku kiboko jike ni wadogo kidogo wakiwa na wastani wa uzito wa kg 1300 – 1500, lakini pia kiboko mkubwa dume anaweza kuwa mkubwa sana hadi kufikia kg 3200 na hata mara kadhaa kufikia kg 4500. Halikadhalika kiboko dume huendelea kukua muda wote wa maisha yao, huku majike hufikia uzito wa juu wakifikia umri wa miaka 25.

Kwa mujibu wa kipindi cha 'Dangerous Encounters with Brady Barr', kupitia Televisheni ya National Geographic Channel, Dk. Brady Barr alipima mkandamizo wa taya za kiboko mara aumapo na ya kiboko jike na kupata kg 826.Aidha, Barr alijaribu pia kupima kwa kiboko dume lakini hakufanikiwa kutokana na ukorofi wa kiboko dume.

Pia kiboko ana urefu wa mita 3.3 hadi 5.2, kujumrisha na mkia wenye urefu wa sm 56, sambamba na pembe kubwa na nywele upande wa kulia kulingana na jinsia yake, na urefu wa karibia mita 1.5 kwenye mabega yake.

Mbali na hayo, licha ya kuwa kiboko ni mnyama mkubwa, na wanauwezo wa kukimbia sana kuliko hata binadamu wakiwa nchi kavu, huku ikikadiriwa kuwa mwendokasi wao ni kutoka km 30 mpaka 40 au hata 50 kwa saa, lakini zaidi ya hayo pia kiboko anaweza akabakia na mwendo huu kwa umbali wa walau mita mia kadhaa tu.

Kiboko huishi kwa miaka 40 mpaka 50. Kiboko aitwaye Donna, anayeishi akiwa na umri mkubwa kuliko wote sasa 57, huko Mesker Park Zoo katika Evansville, Indiana. Kiboko aliyewahi kuripotiwa kuwa na umri mkubwa zaidi aliitwa Tanga, aliishi huko Munich, Ujerumani na alifariki mnamo mwaka 1995 akiwa na umri wa miaka 61. Macho, masikio na pua za kiboko yapo juu ya fuvu la kichwa. Hii huwaruhusu kuzamisha sehemu kubwa ya mwili wao kwenye maji au matope na kupata ubaridi kujizuia na mwanga mkali wa jua.

Mifupa ya kiboko imejengwa kuweza kubeba uzito wa mnyama wote. Kama mamalia wengine waishio majini, kiboko pia wana nywele chache za mwilini.

Ngozi zao hutoa majimaji mekundu kwa ajili ya kuzuia kuungua na jua, majimaji hayo huitwa pia ‘jasho jekundu’, japo si damu wala jasho. Majimaji haya mwanzoni huwa hayana rangi lakini baada ya dakika kadhaa huwa mekundu, na baada ya muda huwa ya kijivu.

Kemikali mbili zimetambuliwa ndani ya mnyama huyu ‘hipposudoric acid’ na ‘norhipposudiric acid’ ambazo zote zina asili ya asidi. Kemikali hizi huzuia ukuaji wa bakteria wanaosababisha magonjwa na pia kusharabu pigmenti za mwanga wa jua aina ya ‘ultraviolet’ na kuziua athari za mwanga wa jua. Na viboko wote hata wanaotofautiana milo yao huwa na kemikali hizi za aina moja, hivyo kemikali hizi hazitokani na chakula.

Mbali na hayo, Mpori pori wa blog hii anakujuza haya mengine zaidi kuhusu Kiboko ‘JE WAJUA!’
Kiboko hupatikana barani Afrika peke yake.

Mtoto wa kiboko huzaliwa akiwa na takribani kilo 30 na huanza kula nyasi baada ya wiki tatu.

Kiboko kwa siku huhitaji takribani kilo 140, na huwa na nyakati mbili za kwenda kujipatia chakula ambapo ni nyakati za asubuhi na usiki.

Kiboko ni nyama alae nyasi tu.

Mtoto wa kiboko huzaliwa ndani ya maji.

Kiboko hutumia meno yao makubwa mawili kujilinda na adui.

Kiboko anauwezo wa kuruka ila anauwezo wakukimbia zaidi ya binadamu, anauwezo wakukimbia kilomita 30 kwa saa.

Kiboko ni mnyama ambaye hunyonyesha mtoto wake kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, huku maziwa yake yakiwa ni ya rangi ya ‘pink’ rangi hii ni kutokana na kuwepo kwa acid mbili ndani ya mwili wa kiboko. Hipposudoric acid” na Norhipposudoric moja ikiwa na rangi nyeupe na huku nyingine ikiwa na rangi nyekundu.

TAHADHARI:
Ni vizuri ukatambua kuwa Kiboko ni miongoni mwa wanyama wakali sana.


Hapa ndipo inapodhihirika wazi mnyama kiboko kweli anambio
Sambamba na hayo, yote wapori pori huwa wana hii story kuhusu kiboko sio mbaya nikashare na wewe leo, Eti “Wakati Mwenyezi Mungu anafanya uumbaji wake wa viumbe vya duniani akiwemo mnyama kiboko mwanzoni aliumbwa kuwa mnyama aishie nchi kavu na sio majini, lakini sasa kiboko kwa tamaa yake alikuwa akiishi kwenye maji, Mwenyezi Mungu akaamua kumruhusu ila akampa masharti kwamba ataenda kuishi kwenye maji ila atakuwa na uwezo wa kula nyama. Hapo ndio hadi leo hii kiboko ukimtizama anaonekana kuwa na meno makali ila anauwezo wakula nyama”

Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel kutoka kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's Ltd, ambao ni mabingwa wa kuandaa safari za kitalii pamoja na kukodisha magari kwa gharama nafuu sana, endapo ungependa kujaribu huduma zao hebu watafute kwa simu namba 0654 022 054 / 0715 437 283 au kupitia www.samscarental.com.

1 comment:

  1. Habari Mkusanyiko: Hivi Unafahamu Kuwa Mnyama Kiboko Hutoa Jasho Linalofanana Na Damu? Tafadhali Twende Sambamba Hapa Katika Jicho Letu Porini >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Habari Mkusanyiko: Hivi Unafahamu Kuwa Mnyama Kiboko Hutoa Jasho Linalofanana Na Damu? Tafadhali Twende Sambamba Hapa Katika Jicho Letu Porini >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Habari Mkusanyiko: Hivi Unafahamu Kuwa Mnyama Kiboko Hutoa Jasho Linalofanana Na Damu? Tafadhali Twende Sambamba Hapa Katika Jicho Letu Porini >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK

    ReplyDelete

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname