WALIMU KENYA WATAKIWA KURUDI KAZINI JUMATATU
Agizo hilo limetolewa baada ya mazungumzo ya siku nzima kati ya chama cha kutetea masilahi ya walimu pamoja na upande wa serikali katika mahakama ya viwanda.
Pamoja na agizo hilo Mahakama hiyo imewaaamuru walimu kurejea kazini na kwamba hakuna anayepaswa kuchukulia hatua za aina yoyote kwani mgomo huo ulikuwa halali.
Serikali pamoja na upande wa walimu zimetakikana kuwasilisha mapendekezo kuhusiana na malipo ambayo walimu wanataka.
Kufuatia agizo hilo la mahakama, walimu wanatarajiwa kurejea kazini Jumatatu huku wazazi na wanafunzi wakipata afueni. Halikadhalika juhudi za hapo awali kujaribu kuzuia mgomo huo hazikufua dafu huku mgomo huo ukiingia katika wiki yake ya pili.
Sambamba na hayo Wabunge pia waliitaka serikali kusuluhisha mgomo huo na kuwapa walimu wanachotaka kwani wanafunzi hawajapata masomo tangu muhula mpya wa shule kuanza nchini Kenya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment