Mwigizaji Irene Uwoya amesema kuwa anataka atambulike nje ya nchi kuliko ndani, licha ya kuwa anajua siyo jambo rahisi kufanya vizuri nje ya nchi, lakini huko ndiko anakotaka kufika.
Uwoya alisema kuwa hivyo inyeshe mvua au liwake jua atajitahidi kuhakikisha kwamba ndoto zake zinatimia.
Uwoya alisema kuwa alijaribu kutengeneza mtandao wa kazi na wasanii wa nje wakati anatayarisha filamu ya ‘Kisoda’ ambayo picha zake zilipigwa nchini Afrika Kusini na Uturuki.
Aidha, Uwoya alifafanua kuwa wakati mwingine siyo lazima kusafiri, kuna wakati wasanii wa nje wanaweza kuja Tanzania kikazi, ujio wao ni nafasi ya pekee kwao, au kwa kufanya nao kazi hapahapa, ama kuchukua mawasiliano na kuwafuata baadaye kwa ajili ya kufanya nao kazi.
“Tena nawaambia wale wote wenye nafasi au wanaofahamiana na watu wanaopenda kwa dhati kufanya kazi na waigizaji wa Tanzania, wasikose kuwaambia hata mimi napenda na ninaweza kufanya hivyo, ” alisema Uwoya.
Muigizaji Irene Uwoya |
Kauli hiyo ya Uwoya imekuja wakati waigizaji kadhaa wakionesha nia kama yake akiwamo Wastara anayenadi filamu mpya ya ‘Mateso wanayopata Watanzania nje ya nchi’ na mwigizaji anayedaiwa kuwa na nguvu ya kukubalika kwenye jamii Wema Sepetu akiwa amerudi juzi kutoka nchini Ghana ambako alikwenda kupiga picha za filamu yake iitwayo ‘After Death’.
No comments:
Post a Comment