Baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete Kumfukuza kazi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka kutokana na kuhusika katika sakata la Escrow na kuahidi kwamba viongozi wengine ambao wanatajwa kuhusika katika sakata hilo atawawajibisha baada ya uchunguzi zaidi kukamilika. Hii ndiyo taarifa iliyotolewa Disemba 23 kutoka Ikulu
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tzFax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD, 11400 DAR ES SALAAM. Tanzania. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni
Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi, Katibu
Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini, ili kupisha uchunguzi wa tuhuma
dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi Sefue amemsimamisha kazi Ndugu
Maswi kuanzia leo, Jumanne, Desemba 23, 2014, kwa kutumia madaraka
aliyonayo kama Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na
Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Balozi Sefue mjini Dar es Salaam imesema kuwa amechukua hatua hiyo “Kwa mujibu wa Kifungu 4(3) (d) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Na. 8 ya mwaka 2002 (kama ilivyorekebishwa)” ambapo “Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mamlaka ya Nidhamu kwa Watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais, wakiwemo Makatibu Wakuu.”
Badala yake, Balozi Sefue amesema kuwa
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi C.
Mwihava atakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini,
hadi uchunguzi dhidi ya Ndugu Eliakim C. Maswi utakapokamilika.
Taarifa hiyo ya Balozi Sefue pia
imekariri kauli ya Rais Kikwete katika hotuba yake kwa Taifa jana,
Jumatatu, Desemba 22, 2014 ambako Rais alisema:
“Kuhusu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, kwa vile ni Mtumishi wa Umma, anatawaliwa
na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma, hivyo nimeshaelekeza Mamlaka
kuchunguza tuhuma zake na hatimaye ikibainika ana makosa hatua za
kinidhamu zitachukuliwa.”
Ndugu Maswi, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu
Ndugu Frederick Werema pamoja na Mawaziri wawili walituhumiwa wakati wa
Kikao cha Bunge kilichopita kuhusiana na Akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakati huo huo, Rais Kikwete ameelekeza
kuwa pamoja na hatua nyingine zinazochukuliwa, Shirika la Umeme
(TANESCO) waendelee na majadiliano na IPTL kuhusu uwezekano wa kushusha
tozo la uwekezaji (capacity charge) zaidi ya punguzo la awali lililopatikana kupitia Kituo cha Kimataifa cha Kusuluhisha Migogoro ya Kimataifa (ICSID).
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Desemba,2014
No comments:
Post a Comment