KUNDI LA ZAMANI LA KAOLE SASA WANAKUJA UPYA NA KUITWA KAONE

Siku chache zimesalia kabla ya kuelekea ule usiku wa Wasanii Wakongwe ambao ni Desemba 26 ‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar es Salaam, mastaa ambao walikuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya litakalojulikana kama Kaone.

Usiku huo unatarajiwa kuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka Kaole kama vile Koletha, Davina, Swebe, Zawadi, Kingwendu, Nyamayao, Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine wengi, ambao kwa mara ya kwanza watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa itakayoanza kuruka hewani Januari 4, mwakani (2015) kupitia kituo cha TV1.



Kulia ni Muhogo Mchungu akifafanua jambo mbele ya wanahabari ambao hawapo pichani, kushoto ni msanii Thea
Wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Kaole wakizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam
Wasanii wakifurahia jambo katika mkutano huo na wanahabari ambao (hawapo pichani)
Aidha, usiku huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, akiwemo Baby Madaha pamoja na Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.

Sambamba na hayo, imeelezwa kuwa kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo, mazingaombwe pamoja na kutoa zawadi nyingi, huku watoto wengine wakipata nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.

Picha zote na Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname