NDEGE YA AIR ASIA SASA YAANZA KUTAFUTWA NA WANAMAJI KUTOKA NCHINI MAREKANI
Kufuatia kupotea kwa ndege ya Shirika la Air Asia wanamaji kutoka nchini Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manowari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu Jumapili katika Bahari ya Indonesi.
Manowari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu sasa tangu kuanza msako dhidi ya ndege hiyo.
Aidha, idadi ya wataalam wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia, Australia, Korea Kusini, Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo.
Naye Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo, amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30, ndege 15 na Helkopta katika eneo la tukio. Ndege hiyo ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment