Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki |
Jiji la Dar es Salaam linaangalia upya uwezekano na utaratibu wa
kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) katika
maeneo yasiyoruhusiwa katika jiji hilo, baada ya sheria na hatua
zinazochukuliwa ikiwemo kuwarudisha ombaomba hao katika mikoa wanayotoka kuonekana
kugonga mwamba na tatizo hilo kuonekana kuendelea kuwa sugu kufuatia wengi wao
kurudi katika maeneo ya awali kila wanapoondolewa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki wakati
alipokuwa akifuangua kikao cha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es Salaam
(RCC) kilichofanyika Desemba 17 jijini Dar es Salaam kujadili masuala
mbalimbali ya mendeleo katika jiji hilo.
Sadiki, alisema kuwa
kuendelea kuwepo kwa wafanyabiashara hao katika maeneo yasiyo rasmi ni
moja ya changamoto inayolikabili jiji la Dar es Salaam kutokana na biashara
wanazozifanya kuchangia kuzuia maeneo ya barabara ya waenda kwa miguu, kusababisha
uchafuzi wa mazingira, kusabisha msongamano wa magari kwa baadhi yao kuweka
bidhaa barabarani.
Aidha, Sadiki aliendelea kusema kwamba, kutokana na hali hiyo baadhi ya
wafanyabiashara walio na biashara rasmi ambao hulipa kodi za Serikali
wamekuwa wakilalamikia hali ya ukwepaji wa kodi inayofanywa na
wafanyabiashara hao.
Wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) wakiwa wamepanga bidhaa zao kandokando ya barabara ya Kawawa jijini Dar es Salaam |
Wamachinga wakiendelea na biashara zao eneo la Karume jijini Dar es Salaam |
Mmoja wa wazee wanaoomba akijaribu kuomba kwa wapita njia |
Mbali na hayo, Sadiki aliongeza kuwa
mpango wa mkoa wa sasa ni kuendelea kuwatumia wafanyabiashara hao
kama fursa ya mtaji wa rasilimali watu ambayo itatumika kama chanzo cha
mapato katika kuleta maendeleo ya mkoa.
Lengo la habarimkusanyiko.blogspot.com ni kuhakikisha unapata habari mbalimbali kutoka kwetu, asante kwa kuwa nasi
No comments:
Post a Comment