Tukio hilo la Bill Gates kunywa maji hayo lilianishwa kupitia kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake, Bwana Bill Gates ambapo alishuhudia kinyesi cha binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.
Bill Gates alisema kwamba ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.
Bill Gates akiwekewa maji ya mradi huo kwenye glass tayari kwa kuonja |
Bill Gates akinywa maji yaliyotengenezwa kutokana na kinyesi cha binadaamu |
Aidha, inaelezwa kuwa teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya mijini, huku shirika hilo likibainisha kuwa takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.
Naye Peter Janick ambaye ni mtengenezaji wa mtambo huo alisema kuwa, maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo na kutengwa na taka ngumu na kuongeza kuwa taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo, na kisha maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.
Source: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment