HUU NDIO UJUMBE KWA WATUMIAJI WA BODA BODA NCHINI



Mwanza
WATUMIAJI wa usafiri wa pikipiki mkoani hapa wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubadili namba za pikipiki zao  kabla ya kufika mwezi Machi 31 mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake afisa huduma wa elimu ya mlipakodi kanda ya ziwa, Lutufyo Mtafya, alisema kuwa hadi hivi sasa wamekwisha kujitokeza wengi katika zoezi hilo.

“kwa kuwa hadi hivi sasa tunaona wengi wakija ofisini inawezekana hadi ifikapo tarehe hiyo ya mwisho tuliyoiweka Machi 31 tutakuwa tumekamirisha zoezi hili, ila wale ambao bado hawajaja waendelee
kuja”,
 alisema Lutufyo.

Aidha, Lutufyo aliendelea kusema kuwa kama kuna baadhi ya watumiaji wa vyombo hivyo wana mashaka na zoezi hilo wafike ofisini hapo kwa kuelimishwa zaidi, huku akieleza kuwa muitikio ni mkubwa kutokana na matangazo waliyoyatoa kuanzaia  mwezi wa tisa mwaka jana.
Madereva bodaboda wakiwa katika foleni ya kujaza mafuta
Hata hivyo, Lutufyo alisema kuwa wanatarajia ndani ya mwezi huu kuwa na semina na wafanyabiashara wa pikipiki pamoja na mabosi, huku lengo likiwa ni kutoa elimu zaidi na ufahamu wa masuala yote yanayohusiana na vyombo vya moto.

“ Tunatarajia mwezi huu kuwa na semina na wafanyabiashara wa pikipiki pamoja na mabosi wao tukilenga kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na vyombo vya moto, na sasa tuko kwenye maandalizi ya semina hiyo”, alisema Lutufyo.

Taarifa hii imeandaliwa na Goodluck Ngowi, ambaye ni mwakilishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com kutoka jijini Mwanza. Tafadhali endelea kuwa nasi kwa taarifa mbalimbali kutoka kila kona ya Tanzania 

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname