Kufuatia kuelekea kufungua kwa shule nchini baadhi ya wazazi mkoani Mwanza wamelalamika kupanda kwa bei za vifaa vya shule.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na mwandishi wa habarimkusanyiko blog, wazazi hao walisema kwamba kila mara kumekuwa na tabia ya kupandishwa kwa bei ya vifaa hivyo hususani inapofikia wakati kama huu wa shule kufunguliwa.
Mmoja wa wazazi hao Anna Hamis, alisema hawafurahishwi na vitendo hivyo kwani wamekuwa wakipata wakati mgumu katika kutafuta mahitaji ya watoto wao na kuziomba mamlaka husika kusimamia suala hilo ambalo limekuwa likizidi kuota mizizi siku hadi siku.
Naye John Masuke, ambaye pia ni mnunuzi alisema suala hilo si la kulifumbia macho na kuitaka Serikali ichukue tahadhari mapema kabla halijazoeleka kama inavyochukua hatua katika biashara nyingine.
‘’Serikali lazima iangalie suala hili na kulidhibiti mara moja kama ilivyofanya katika vyombo vya usafiri” alisema Masuke.
Aidha, kwa upande wao baadhi ya wauzaji wa vifaa hivyo walisema wao wamekuwa wakiuza kulingana na bei wanayonunulia kutoka kwa mawakala wao, huku wakiongeza kuwa hawana sababu ya kupandisha bei kwa wateja wao.
‘’Wateja wetu tunawapenda, wao ndio wanatufanya tukae hapa kwa ajili ya biashara, sisi hatupandishi ila mawakala wetu wanapandisha hali hii inatufanya na sisi tupandishe bei’’ alisema Asenga.
Habari hii imeandaliwa na Goodluck Ngowi mwakilishi maalum wa habarimkusanyiko blog kutoka jijini Mwanza na mwenye jukumu la kuhakikisaha wewe msomaji wetu unapata story zote kutoka kanda ya ziwa. Asante kwa kuwa nasi msomaji wetu.
No comments:
Post a Comment