Ni wazi kwamba watu wengi kwa sasa wamekuwa wakitumia mitandao mbalimbali katika kuwasiliana na watu tofauti tofauti ulimwenguni, lakini hii inaweza ikawa funzo kwako wewe ambaye ni mtumiaji wa mitandao, ambapo inaelezwa kwamba kijana mmoja nchini Uingereza mwenye mienendo ya kustaajabisha hivi karibuni alipiga simu kwa polisi na kuwaarifu kuwa amemchinja kijana mwenzake mwenye umri wa miaka 14 ambaye walifahamiana kupitia mtandao.
Kijana huyo alipigia simu polisi na kuwaambia kwamba angependa waende nyumbani kwake huku wakiandamana na wataalam wa uchunguzi wa mauaji kwani alikuwa amemuua rafiki yake.
Kijana huyo aitwaye Lewis Daynes, mwenye umri wa miaka19, ametajwa na polisi kuwa kijana hatari, mhalifu ambaye anawahadaa wenzake na kisha kuwadhuru.
Taarifa zinaeleza kuwa ilikuwa mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana uso kwa uso kwani siku zote walikuwa wakiwasiliana kupitia internet, lakini baadaye Daynes alimwalika Bednar nyumbani kwake baada ya kujuana tu kupitia internet, huku akimwambia alitaka sana kumuona, lakini Bedner alipowasili nyumbani kwa Daynes, Daynes alimfunga mikono yake na kisha kumuua.
“Ninahitaji polisi kuja nyumbani kwangu,'' alisema kijana huyo na alipoulizwa ikiwa alikuwa anakiri kufanya mauaji akaseme, '' Ndio, ninakiri. ''
Inaarifiwa kuwa baadaye Dynes aliwapa polisi taarifa zake, jina lake na alikoishi na kisha kuwashukuru. Huku akidai kwamba alimuua rafiki yake Breck baada ya kumtisha kwa kisu.
''Sikumbuki kilichotokea, lakini nilimchinja,'' aliwaambia polisi.
Kufuatia taarifa hiyo inaelezwa kwamba baadaye polisi walifika nyumbani kwake na kumpata Daynes akiwa mtulivu huku mwili wa rafiki yake ukiwa sakafuni.
Daynes, ametajwa kama kijana ambaye hakueleweka kitabia ila alipenda sana kutumia muda wake kwenye kompyuta. Wazazi wake waliachana hali iliyosababisha maafisa wanaoshughulika maslahi ya watoto kumpeleka kwa familia ambayo sio yake ili aweze kutuzwa.
Hata hivyo, Daynes ili kufuta ushahidi wa mauaji hayo inaelezwa alikatakata nguo alizokuwa amezivaa na akijaribu kuharibu kompyuta aliyokuwa anaitumia ili kufuta ushahidi wa mazungumzo waliyokuwa nayo na rafiki yake kabla ya kumuua.
Mbali na hayo, inaarifiwa kuwa kabla ya kuwapigia polisi simu, Daynes alimtumia mtu mmoja picha ya mwili wa Bednar kama ushahidi wake kwamba amemuua. Hata hivyo polisi bado wanachungaza ili kumtambua mtu huyo.
Sambamba na hayo, mama yake na kijana aliyeuawa amesema anatumaini kuwa kisa cha mwanake kitakuwa funzo kwa vijana wanaojihusisha na michezo ya kwenye internet, huku akisema kwamba vijana wanapaswa kuchungua tahadhari wanapojihusisha na maswala ya mitandao
Source:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment