UFARANSA YAFANYA MAANDAMANO KUONESHA UMOJA WAO KUFUATIA TUKIO LA KIGAIDI LA HIVI KARIBUNI
Rais wa Ufaransa Francois Hollande hapo jana ameongoza maelfu ya watu kwenye mitaa ya Paris, ikiwa ni kuonesha umoja na waathiriwa wa shambulizi la kigaidi la Januari 7 lililouwa watu 17.
Katika maandamano hayo, viongozi wa dunia waliungana na Bwana Hollande katika mji mkuu wakati kundi la watu likihamasisha umoja kwenye maandamano kote katika mitaa.
Miongoni mwa viongozi wa dunia walioshiriki katika maandamano hayo ni pamoja na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron , Kansela wa Ujerumani Angela Markel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas pamoja na mfame na mama mfalme wa Jordan.
Mbali na hayo, maafisa wa Ufaransa wameita mauaji ya Januari 7 katika ofisi za Paris kwenye gazeti la Charlie Hebdo na mfululizo wa mashambulizi mengine ya mauaji ni ya kigaidi.
Wakati huo huo mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder alitangaza kwamba rais Barack Obama atakaribisha viongozi wa dunia mjini Washington, February 18 katika mkutano wa kupinga ghasia zenye msimamo mkali.
Ni dhahiri kuwa tunafarijika kuendelea kuwa nawe msomaji wetu wa habarimkusanyiko.blogspot.com, tafadhali endelea kuwa nasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment