VYOMBO VYA HABARI VYATAKIWA KUTOA ELIMU KUHUSU KATIBA INAYOPENDEKEZWA
Serikali imetoa wito kwa vyombo vya habari hapa nchini kuwaelimisha wananchi kuhusu Katiba inayopendekezwa ili waweze kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kuipigia kura.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh. Dkt Fenella Mukangara wakati alipokuwa akifungua kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini kinachofanyika Mkoani Mtwara.
Aidha, Dkt Mukangara amewataka Maafisa Mawasiliano Kushirikiana na vyombo vya habari katika kuielimisha jamii kuhusu Katiba nayopendekezwa ili wananchi waweze kufanya uamuzi sahihi wakati wa kupiga kura ya maoni.
Hali kadhalika Dkt Mukangara alizungumzia swala la wananchi kujiandisha ili wapate fursa ya kupiga kura ya maoni, ambapo amesema ni vyema Maafisa Mawasiliano wakashirikiana na vyombo vya habari kuwahamasisha wananchi kujiandisha kwa wakati muafaka pia.
Pamoja na hayo, Waziri Mukangara alisisitiza kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuimarisha uhuru wa wajibu wa vyombo vya habari pamoja na wajibu wa Maofisa Mawasiliano kutoa taarifa kwa umma ndio maana imeandaa kikao kazi hicho.
Aidha, Dkt. Fenella alisema kuwa ushirikiano kati ya Maafisa Mawasiliano Serikalini na Wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini utasaidia kutafuta namna bora ya kutoa habari kwa umma na kwa usahihi na weledi unaohitajika.
Kikao hicho kinafanyika Mkoani Mtwara kuanzia Januari 26,hadi Februari Mosi 2015 katika ukumbi wa NAF Hotel Mkoani Mtwara kikiwashirikisha wahariri wa vyombo kutoka vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment