WANANCHI JIJINI MWANZA WANATARAJIWA KUPATIWA MAFUNZO YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA




WANANCHI jijini Mwanza wanatarajia kupata mafunzo ya namna ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya, jambo ambalo limekuwa ni tatizo kwa Taifa, huku likioneshwa kuchangiwa na ukosefu wa elimu juu ya athari za madawa hayo.

Hayo yalisemwa na katibu mtendaji wa Rafiki Family Foundation Deodory John, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, kupitia mradi wa Waungwana project (WAP).

Aidha, John aliongeza kuwa lengo la kuanzisha mradi huo ni kupunguza matumizi ya dawa za kulevya, kutokana na ongezeko la matumizi hayo kuchangia kudhorotesha afya za vijana pamoja na kupoteza nguvu kazi, jambo linalochangia pia kushuka kwa kiwango cha uchumi.
 
“Tumeanzisha mradi huu kutokana na matumizi ya dawa za kulevya kuongezeka kwa kasi maeneo mengi ya jiji la Mwanza na kusababisha madhara kiafya kwa watumiaji, huku baadhi yao wakichangia sindano katika matumizi ya madawa hayo jambo linaloweza kusababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi, na kupelekea uchumi wa nchi kuyumba kutokana na vijana kupoteza muda mwingi katika matumizi ya dawa,” alisema John.


John aliendelea kusema kuwa suala la madawa ya kulevya limekuwa changamoto kwa taifa kutokana na na kutokuwapo kwa utaratibu wa kuwapatia watu elimu hiyo tangu wakiwa shule ya msingi, hivyo
wanatarajia mafunzo hayo kuyaingiza katika mitaala ili iweze yaweze kuanza kutolewa kuanzia ngazi ya elimu ya msingi mpaka chuo, jambo litakalosaidia jamii kujua madhara na njia ya kijitibu na kujinusuru na matumizi ya dawa hizo.

Hata hivyo, John aliiomba serikali kuwapatia eneo la kujenga kituo cha kutolea mafunzo na tiba kwa walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya na kupatiwa vitendea kazi, ili kupunguza tatizo hilo kwani wataalam waelimu ya dawa za kulevya ni wachache, tofauti na watumiaji.

Pamoja na hayo, aliiomba jamii na serikali kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi ya dawa za kulevya, huku akiitaka serikali iwakutanishe na wadau mbalimbali watakao wasaidia katika suala zima la uelimishaji juu ya matumizi hayo na madhara yake.

Mbali na hayo, John alisema kuwa pia katika mafunzo hayo yatahudhuriwa na watu wote wakiwemo walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya, huku akibainisha kuwa mafunzo hayo yatagharimu kiasi cha shilingi sh100000 kwa wiki mbili awamu ya kwanza,lakini alisema gharama hizo ni kutokana na kutokuwa na wadhamini wa kuwawezesha katika zoezi la uelimishaji huo, hivyo wakipata muwezeshaji mafunzo hayo yatatolewa bila gharama yoyote.

Story hii imeandikwa na Goodluck Ngowi, ambaye ni mwakirishi wa habarimkusanyiko kutoka jijini Mwanza, Asante kwa kuendelea kuwa nasi msomaji wetu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname