KUHAMA KWA MAKUNDI YA WANYAMA NI MOJA KATI YA VIVUTIO VINAVYOPATIKANA KATIKA BARA LA AFRIKA, SOMA ZAIDI UJUE NA VIVUTIO VINGINE
Ikiwa bado Jicho La Pori likiendelea kulichambua Bara la Afrika na vivutio vyake.
Itakumbukwa kwamba mwaka 2013 katika mkoa wa Arusha, Tanzania kuliwezakufanyika mkutano wa kupendekeza vivutio saba vya kiasili vilivyopo barani Afrika.
Sasa nimeona leo nikujuze au kukufahamisha vifutio hivyo vilivyo pendekenzwa katika mkutano huo.
Uhamaji wa wanyama katika hifadhi ya Serengeti
Hivi unafahamu kuwa kila mwaka takribani nyumbu 1.5million, pundamilia 400,000 na swala 200,000 huama na kuelekea nchni Kenya katika hifadhi ya Masai Mara na kurudi tena Serengeti. Basi huo ndio uhamaji mkubwa na mrefu wa wanyama katika dunia nzima.
Neno Serengeti ni neno la kimasai ilikiwa na maana ya aridhi isiyo na mwisho.
Ngorongoro kreta, hii ndio hifadhi pekee ambayo binadamu pia ameruhusiwa kufanya shughuli zake kama uchungaji wanyama hali kadhalika hii ni hifadhi yenye wanyama pori zaidi ya 30,000 wakiwemo faru.
Ngorongoro kreta inaupana wa 19.2 km na mita 610 kwenda chini.
Mlima kilimnjaro, huu ni mlima mrefu kuzidi yote barani Afrika, unaurefu wa mita 5,895 na ni mlima wenye volcano iliyolala kwa sasa
Mlima huu una vituo saba hadi kufika kwenye kilele huku uhuru ndio kituo cha juu kabisa
Mto nile ndio mto mrefu dunia wenye urefu wa kilomita 6,650 na unakatiza katka nchi takribani kumi, huku ukimwaga maji yake katika nchi ya misri.
Jangwa la sahara, ni jangwa kubwa duniani na limechukuwa takribani nchi 11, huku likiwa na kubwa wa kilomita za mraba 9,000,000 na vifusi vya mchanga vinatakribani mita 180
Delta ya okavango, hupatikana nchini Botswana na maji yake hutapakaa takribani kilomita za mraba 6,000-15,000.
Bahari ya shamu, ni ghuba kubwa ya Bahari Hindi Jina la kihistoria katika lugha ya Kigiriki ilikuwa Bahari ya Eritrea. Ghuba yote ina urefu wa takriban 2000 km na upana wake ni kati ya 300 km na 20 km tu kwenye Bab el Mandeb.
Pia eneo lake ni 450,000 km² na ni bahari yenye aina za samaki takribani 1,200.
Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel kutoka kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's Ltd, ambao ni mabingwa wa kuandaa safari za kitalii pamoja na kukodisha magari kwa gharama nafuu sana, endapo ungependa kujaribu huduma zao hebu watafute kwa simu namba 0654 022 054 / 0715 437 283 au kupitia www.samscarental.com.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment