HAYA NDIO MAAMUZI MENGINE YA MHESHIMIWA KINGWANGALA



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza Watanzania wote kutokubali kutozwa rushwa kwa ajili ya damu salama na baadala yake kwa mtu atakayefanya hivyo atachukulia hatua kali za kisheria.


Kauli hiyo imetolewa na Dkt. Kingwangalla alipofanya ziara katika Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dares Salaam.



Afisa uendeshaji wa wa ofisi ya mpango wa Taifa wa damu salama zilizopo jijini Dar es Salaam Bw. Abdu Juma akimuonesha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamisi Kigwangalla moja ya damu ambayo ni maalum kwa kinamam wajawazito wakati wa kujifungua zilizohifadhiwa kwenye jokofu katika maabara hiyo
Aidha, Dk. Kigwangalla katika kusisitiza hilo amesema nesi au daktari ama mtaalamu wa afya, atakayemtoza mtu damu, atachukuliwa hatua kali ikiwemo kufukuzwa kazi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname