MTOTO WA RAILA ODINGA AFARIKI DUNIA




Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, Fidel Odinga amekutwa akiwa amefariki nyumbani kwake huko Karen.

Kufuatia kifo hicho maafisa wa polisi tayari wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha kijana huyo wa Odinga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara pamoja kuonekana katika ulingo wa kisiasa pia.

Hata hivyo, maafisa wa Polisi wanasema kuwa uchunguzi wa mapema umeonesha kuwa Fidel alikuwa nje usiku wa Jumamosi na alirudi mapema Jumapili, lakini bado haijafahamika ni nini kilichosababisha kifo chake.

Pamoja na hayo Maafisa wanaosimamia kesi hiyo wanasema kuwa wanataka kujua ni wapi Fidel alikuwa usiku wa Jumamosi na alikuwa na nani.

Sambamba na hayo, taarifa zinasema kwamba kundi la wabunge pamoja na maseneta liliwasili katika nyumba ya Raila baada ya kupata habari hizo.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname