MWANAFUNZI AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA JELA KWA KOSA LA KUMTUKANA RAIS


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.

Mwanafunzi huyo aliyefahamika kwa jina la Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25, mbali na adhabu hiyo pia atatakiwa kulipa faini ya dola 2,200 la sivyo atatumikia kifungo kingine cha mwaka mmoja.

Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la Kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.

Itakumbukwa kwamba humo humo nchini Kenya Mwanablogu mashuhuri pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname