FAHAMU VITU 15 KUHUSU MNYAMA TEMBO,A MBAVYO HUKUWAHI KUVIFAHAMU AWALI



Karibu msomaji wetu katika “Jicho Letu Porini”, ambapo leo tutaangazia kuhusiana na mnyama Tembo, Mnyama huyu hufahamika pia kwa jina la ndovu au kwa lugha ya kigeni huitwa Elephant, lakini pia jina lake la kisayansi hufahamika kama Loxodanta Africana.
Tembo ndio mnyama pekee ambaye ni mkumbwa kuliko wote anayepatikana ardhini na inaelezwa kwamba tembo dume mkubwa  huweza fikia takribani kilo 2000 – 6000 (Tan 2- Tan 6) huku jike akiwa na kilo 2000-4000 (Tan2-Tan4).Mbali na hayo mtoto wa tembo huzaliwa akiwa na kilo zisizo pungua 120.
Jambo lingine ambalo tungependa ufahamu kutoka Jicho Letu Porini leo ni kuhusu mnyama huyu, ni kwamba kuna spishi mbili za tembo yaani kuna tembo wa Afrika na tembo wa Asia.

Kuna mengi ambayo humuhusu mnyama huyu na ambayo huwezi kuyakuta kwa mnyama mwingine wa porini miongoni mwa hayo mengi ni pamoja na haya yafuatayo…


  •       Tembo wanahuwezo wakusikilizana umbali wa kilomita 8.
  •      Tembo wa Afrika wanahisia nzuri kuliko mnyama yoyote.
  •   Tembo huogopa nyuki.
  • ·   Ukiacha na binadamu, tembo ndio mnyama mwenye kidevu.
  • ·   Tembo ni mnyama ambaye hulala mda usio pungua masaa mawili hadi matatu kwa siku.
  •    Tembo huhitaji takribani kilo 300 kwa siku na lita 160 ili kumuwezesha kushiba, na chakula chake ni majani, magome ya miti, mizizi pamoja na matunda.
  •   Tembo ndio mnyama pekee anayebeba mtoto tumboni (mimba) kwa kipindi cha muda mrefu kuzidi wote dunia ni miezi 22, na mtoto hutoka mmoja tu.
  • ·  Tembo hushika mimba kila baada ya miaka miwili
  •     Meno ya tembo hukaliliwa kufika kilo 200 (yote mawili)
  • ·   Kundi la tembo au Familia ya tembo huongozwa na jike
  •     Tembo ni mnyama mwenye kumbukumbu nzuri
  •    Tembo akiwa porini huweza kuishi takribani miaka 60-65.
  •  Tembo anaanza kutokwa na meno ya nje baada ya miezi kumi na sita ila ifikapo miezi 30 ndio huuanza kuonekana.
  •   Kinyesi cha tembo huaminika kuwa ni dawa.
  • Tembo ni miongoni mwa wanyama anayepatikana katika hifadhi zetu hapa nchini yapaswa kujivunia na kuwatunza kwa faida ya vizazi vijavyo pia

Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel muongozaji wa watalii kutoka kampuni ya Sam’s Car Rental Tour & Safar’s  Ltd, hivyo tunakusihi kuungana nasi ili ufahamu mengi pia kuhusu maisha ya wanyama.

6 comments:

  1. It's good and wonderful about elephant am jafeti Julius from sokoine University of agriculture am persuing bachelor of tourism Management it's gud you will contact in this whassp no 0757175511 so as I can learn much from you

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download Now

      >>>>> Download Full

      Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download LINK

      >>>>> Download Now

      Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download Full

      >>>>> Download LINK Sw

      Delete
  2. Safi sana! Nimejifunza kitu kuhusu tembo.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Kwa Elimu nzuri sans

    ReplyDelete
  4. Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Habari Mkusanyiko: Fahamu Vitu 15 Kuhusu Mnyama Tembo,A Mbavyo Hukuwahi Kuvifahamu Awali >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK

    ReplyDelete

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname