ALI KIBA AFUNGUKA KUHUSU BIFU YAKE NA DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa muziki wa Bongo fleva, Alikiba ameamua kuweka mambo bayana juu ya bifu yake na staa mwenzake wa muziki huo huo Diamond Platnumz, ambapo Alikiba alisema ni kweli wamekuwa katika bifu hiyo zaidi ya miaka mitatu sasa.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akizungumza na gazeti la Mwananchi, ambapo alisema, tofauti zao hizo zilianza tangu mwaka 2012, lakini cha ajabu zaidi wakati Alikiba akieleza uwepo wa bifu hiyo kwa upande wa pili wa Diamond yeye amekuwa akisikika mara kadhaa akisema kuwa hana tofauti yoyote na mwanamuzi huyo ambaye wanatoka mkoa mmoja wa Kigoma na kuunganishwa Kundi la Kigoma ‘All Stars’.

Aidha, alipotakiwa kujibu endapo aliwahi kuwa na ukaribu wowote na Diamond Alikiba alijibu kuwa “hapana yeye ndiyo alishawahi kuwa na ukaribu na mimi” 

Kuhusu suala la kufanya Kolabo na msanii huyo Alikiba alisema kuwa “sidhani kama ninaweza kuja kufanya kolabo na Diamond, ila nikipata wimbo ambao nadhani kwamba anastahili kuwapo, kiukweli nitamshirikisha, lakini kama hastahili haitawezekana.” 

Akifafanua zaidi kuhusu hilo la kolabo Alikiba aliendelea kusema kuwa “kama mtu anataka kufanya Zouk akimtafuta Stara Thomas itawezekana kwani hayo ndiyo mambo yake, kwa hiyo kama nikitaka kufanya naye wimbo ambao nitaona kwamba unafaa nitamfuata na nitamweleza”
Hata hivyo, Ali Kiba alipohitajika kuelezea utofauti wake kati ya mziki wake na wa Diamond alisema kuwa, “mimi naimba muziki mzuri na nina ‘Hit Song’, naye Diamond anaimba ‘hit song’,

Pamoja na hayo, kuhusu masuala ya kutumia imani za kishirikina Ali Kiba alibainisha kuwa yeye anamuamini Mungu na hana imani hizo kabisa na mimi naamini Mungu na mambo ya hirizi na mimi ni tofauti.

1 comment:

  1. Habari Mkusanyiko: Ali Kiba Afunguka Kuhusu Bifu Yake Na Diamond Platnumz >>>>> Download Now

    >>>>> Download Full

    Habari Mkusanyiko: Ali Kiba Afunguka Kuhusu Bifu Yake Na Diamond Platnumz >>>>> Download LINK

    >>>>> Download Now

    Habari Mkusanyiko: Ali Kiba Afunguka Kuhusu Bifu Yake Na Diamond Platnumz >>>>> Download Full

    >>>>> Download LINK

    ReplyDelete

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname