KUTANA NA PICHA ZA MELI KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI


Hivi karibuni meli kubwa kuliko zote duniani, inaelezwa kuwasili nchini Uingereza na kusababisha kuwa jambo la kivutio kwa baadhi ya wakazi wa nchi hiyo.

Meli hiyo inayoelezwa kuwa ni ya mizigo na yenye uwezo wa kubeba makontena yapatayo 19,100, huku ukubwa wake ukifananishwa na usawa na viwanja vinne vya mpira wa miguu.

Hata hivyo, taarifa zaidi juu ya meli hiyo zinasema kwamba meli huyo imesajiliwa Hong Kong na ilitengenezwa nchini China na inauwezo wa kubeba tani zipatazo 57,000 ambao ni uzito mkubwa zaidi unaoweza kuchukuliwa na chombo cha usafiri duniani.


Pamoja na hayo, taarifa ziliendelea kusema kwamba meli hiyo hadi kuwasili nchini Uingereza ilitumia mwezi mzima kutoka Shanghai China hadi kuwasili nchini humo.
Tunashukuru kwa kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com, karibu tena kwa taarifa nyingine zaidi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname