MESSI ATEGWA NA MKATABA MNONO WA MIAKA 6 KUTOKA CHELSEA



Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna mkataba mnono wa miaka sita kutoka kwa klabu ya Chelsea unaomngojea.

Hii ni kwa mujibu wa duru za karibu na mchezaji huyo wa Barcelona ambapo zinaarifu kuwa Chelsea imeweka wazi kwamba iko tayari kutoa kitita cha pauni millioni 200 kwa lengo la kumnunua nyota huyo.

Aidha, ‘The Blues’ imedai kwamba iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango hicho mara mbili.

Itakumbukwa kwamba mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha klabu hiyo na Messi, lakini katika klabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis Enrique.
Mmiliki wa klabu ya Chelsea Abramovic
Hata hivyo, inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika mazoezi ya siku ya Jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati yake na Messi.
Asante kwa kuendelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com,tafadhali endelea kuwa nasi

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname