PICHA RASMI YA RAIS MAGUFULI TAYARI IMETOKA IPO HAPA

Picha rasmi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli imeshatoka katika ofisi ya idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa kuwa picha hiyo itauzwa kwa shilingi 15,000 ya kitanzania bila ya kuwekwa fremu, huku picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere itauzwa kwa shilingi 5000/=


Bi Kawawa amesema nakala za picha hiyo zinapatikana Idara ya Habari Maelezo na ofisi za wakala wa huduma ya ununuzi serikalini (GPSA).

Mbali na hayi Bi Kawawa amesema picha hiyo ya Rais pamoja na ya baba wa taifa zinatakiwa kutundikwa katika ofisi zote za Serikali, Taasisi za Umma, Maashirika na Taasisi binafsi.

Naye Mkurugenza msaidizi wa habari maelezo Raphael Hokororo amesema picha hiyo ya Rais Magufuli imwahi kutoka kuliko picha za waheshimiwa wote waliopita na kusema kuwa hairuhusiwi kukopi au kunakili picha hiyo.
i
Hokororo pia ametoa onyo kwa wote wanaosambaza picha isiyo rasmi na wale wote wanaotengeneza picha yenye ukubwa usio rasmi nakusema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

"Idara ya Habari Maelezo pekee ndiyo yenye hakimiliki ya picha picha hiyo," alifafanua Bw. Hokororo

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname