KWA WEWE UNAYEPENDA KULA NDIZI MCHEMSHO NI VYEMA UKASOMA HAPA




Ndizi ni moja ya chakula kinachopendwa sana na watu wengi, lakini kwa hapa nchini chakula hiki huongoza kwa kuliwa zaidi na watu wa kabila la Wahaya kutoka mkoa wa Kagera, Bukoba. Sasa leo katika mapishi tutaandaa ndizi mchemsho twende sote...

MAHITAJI

  • Nyama robo

  • Ndizi mzuzu mbichi 5 au kulingana na ukubwa wa familia yako

  • Vitunguu maji

  • Giligiliani vijani kiasi

  • Vitunguu swaumu

  • Rosemary (vijani vichache)

  • Bay (vijani kiasi)

  • Karoti

  • Chumvi

  • Oliver oil kijiko cha mezani kimoja

  • Black pepper

  • Chills endapo unapenda

NAMNA YA KUANDAA

  • Menya ndizi zako na uzioshe vizuri kwa maji safi na salama.

  • Katakata vitunguu maji, na karoti kwa mtindo uupendao

JINSI YA KUPIKA
  • Chemsha nyama na ikiashaiva vizuri weka chumvi kiasi, bay, rosemary, black paper vyote hivi utaweka wakati nyama ikiendelea kuchemka.
  • Nyama ikishaiva vizuri weka vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na nndizi kisha acha viive vyote kwa pamoja, lakini kabla ya kutoa weka karoti.

Baada ya dakika 5 unaweza kutoa chakula motoni na kitakuwa ni tayari kimeiva na unaweza kula mchana au usiku pia.


Pishi hili limeletwa kwenu na kuandaliwa na Asha Habibu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname