AUNT EZEKIEL AFUNGUKA UKWELI WAKE KUHUSU UJAUZITO WAKE


Muigizaji wa filamu Aunt Ezekiel Grayson amepinga vikali kuhusu tetesi za ujauzito wake kuhusishwa na waziri wa sasa wa maliasili na utalii, ambapo mrembo huyo amesema suala hilo limekuwa likimtesa sana moyo wake.
Hata hivyo, mbali na tetesi za ujauzito pia kumekuwa na uvumi kuwa staa huyo alienda nchini Marekani na mheshimiwa huyo. kuhusu hilo Aunt alisema yote anayapuuza na anachojua yeye alienda kwa sababu ya kazi yake ya sanaa.

Aunt alinukuliwa akisema kwamba “kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu ambaye ndiye mhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?”

Aidha, aliendelea kusema kwa uchungu mkubwa kuwa “kweli mimba yangu siyo ya waziri, ifahamike kuwa namheshimu sana mheshimiwa, najisikia vibaya mtu anapoeneza kitu cha namna hiyo,”
Aunt Ezekiel
Pamoja na hayo Aunt alisema alishangazwa na baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.

Kuhusu hilo mrembo huyo alisema kuwa “hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?”
Kutokana najambo hilo kuzungumziwa hadi bungeni aunt anasema kuwa “wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,”.


Sambamba na hayo staa huyo wa filamu hapa bongo alimalizia kwa kusema kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito, huku yakiwa hayana chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo ambaye pia ni mbunge.

Mbali na ishu hiyo ya waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimb aliyonayo si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo kama wengi wanavyodai.Licha ya kuwa Mose Iyobo yeye amekuwa akidai kuwa ujauzito ni wa kwake.
Endelea kuungana nasi kila siku kwa habari moto moto!!!

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname