KIJANA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUCHOMWA KISU SHINGONI AKIWA ANAAMULIA UGOMVI


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Francis Losioku amefariki dunia baada ya kuchomwa na kisu na kaka yake sehemu ya shingo upande wakulia na mtuhumiwa kukimbilia kusiko julikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas, amesema kuwa mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Amoni Losioku (32) mkazi wa Murieti anatuhumiwa kumuua nduguye Francis Losioku siku ya Disemba 5 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku tukio lililotokea baada ya marehemu kuamua ugomvi uliokuwepo kati ya mtuhumiwa na mama yao mzazi.

Aidha, Sabasi amesema kuwa taarifa za awali zilionesha kuwa marehemu alichomwa kisu kutokana na kuamulia ugomvi uliokuwepo baina ya mama yao mzazi na mtuhumiwa Amoni Losioku

Ugomvi huo unaelezwa kusababishwa na mama mzazi baada ya mtuhumiwa kumtuhumu mama yake huyo kuwa ndiye chanzo cha kumfanya mke wa mtuhumiwa kuwa na kiburi, lakini pia mtuhumiwa alionekana kumtupia lawama mama yake kwa kudai kuwa amekuwa akiingilia swala lao la ndoa yake.

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa wakati wa harakati za kuokoa maisha ya Francis Losioku (marehem) baada ya kuchomwa kisu, habari zinasema kuwa walipokuwa wakimuingiza kwenye gari ili wampeleke hospitalini, ambapo walikuwa wakitumia gari la jirani yao aliyefahamika kwa jina la Alfayo Siatoy (46) ambaye pia ni mkazi wa Murieti mkoani Arusha kwa bahati mbaya harakati wakati majeruhi alkipelekwa hospitalini ambaye sasa ni marehemu baba mzazi wa majeruhi aliyefahamika kwa jina la Losioku Vaneti ( 70) ajali ilitokea baada ya shuka lake kunasa kwenye mlango wa nyuma wa gari na kusababisha kuvutwa na gari hilo na kisha kujigonga kwenye bodi ya gari na kupelekea kifo chake.

Sambamba na hayo, Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Sabas, amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kuhusiana na tukio hilo, ikiwa ni pamoja na kumtafuta mtuhumiwa Amoni Losioku, ili atapopatikana awezekuchukuliwa hatua za kisheria, huku miili ya marehemu ikiwa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi.

Habari hii imeandaliwa na  Theo.M. George, ambaye ni mwakilishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com kwa mkoa wa Arusha 

Asante kwa kuendelea kuwa nasi, tafadhali washirikishe ndugu jamaa kuhusiana na uwepo wa blog hii.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname