MTOTO AFANYIWA UKATILI KWA KUINGIZWA MWIKO SEHEMU ZA SIRI, KWA KILE KILICHODAIWA ALIKOJOA KITANDANI



Ikiwa ni siku chache zimepita tangu habarimkusanyiko.blogspot.com turipoti taarifa ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha kuendelea kufanya msako mkali juu ya ukatili uliofanywa dhidi ya mtoto aliyetupwa na kukatwa kiwiliwili na miguu.

Taarifa zinasema kuwa mtu mwingine anashikiliwa na Jeshi hilo la Polisi baada ya kumshambulia mtoto mwingine (jina tunalo) kwa kumpiga na mwiko kichwani kisha kumwingiza mwiko sehemu za siri (njia ya haja ndogo).

Jeshi la Polisi limesema kuwa, mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la Merina Fares Shafii (25) mkazi wa Kijenge alikamatwa mnamo Disemba 5, mwaka huu baada ya kufanya ukatili huo na kumsababishia maumivu makali mtoto huyo.

Aidha Taarifa za awali zinaeleza kuwa, sababu ya mtoto huyo kushambuliwa na mtuhumiwa ni baada ya kujikojolea, hali iliyopelekea kupigwa sehemu za kichwani na kuingizwa mwiko huo sehemu ya haja ndogo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi linafanya taratibu za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo, huku hali ya mtoto huyo ikielezwa kuendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya mkoa ya Mount Meru.

Habari hii imeandikwa na kuandaliwa na Theo M. George ambaye ni mwakilishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com kwa mkoa wa Arusha

Unastahili kuyapata yote haya, na hii ndiyo sehemu sahihi ya kupata habari makini, tafadhali endelea kuwa nasi.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname