FAHAMU ALICHOKISEMA JOKATE KUHUSU KUIGIZA SINI ZA MAPENZI




Mwigizaji wa filamu na mwanamitindo maarufu nchini, Jokate Mwegelo amesema kuwa huwa hapendi kuigiza sini za mapenzi hasa zile anazotakiwa kushikwashikwa na mwanaume hasa asiyemjua.

Jokate aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na paparazi wa GPL mara baada ya kuhitaji kujua namna ambavyo wazazi na mpenzi wake wanavyolipokea suala la yeye kuigiza sini za kushikwashikwa na wanaume tofauti katika filamu hapo ndipo alipofunguka kuwa suala hilo limekuwa likipigwa vita na wazazi wake, lakini analazimika kufanya kwa sababu ndiyo kazi aliyoichagua.

Jokate alisema kwamba “wazazi wangu wanachukia sana jambo hili na huwa wanasema bora niache filamu, hata mimi mwenyewe huwa sipendi ila huwa navumilia kwa kuwa ni kazi, sina jinsi,”

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname