LULU:SIJUTII KUSHINDWA KUOLEWA MWAKA 2014



Mwigizaji Elizabeth Michael maarufu ‘Lulu’ ameibuka na kuelezea ni jinsi gani anavyo lichukulia swala la lengo lake alilojiwekea la kuolewa mwaka 2014 kushindikana na kusema kuwa imeshindikana, lakini hajilaumu wala hamlaumu mtu yeyote kwa kutotimiza suala hilo kwani anaamini Mungu ndiye anayewezesha kila kitu.

Aliyabainisha hayo hivi karibuni wakati akizungumza na paparazi wa GPL, ambapo Lulu alisema mwaka 2014 alikuwa na malengo mengi likiwemo suala la ndoa, lakini kwa kuwa Mungu ndiye muweza, atapanga upya suala hilo na anaamini litakuja kutimia.

“Ndoa ni mipango ya Mungu, huwezi kulazimisha hata siku moja, sisi wanadamu huwa tuna mipango yetu lakini ili ifanikiwe lazima kuwe na baraka za Mungu,” alisema Lulu.


Aidha, Lulu aliendelea kusema kuwa mwaka huu na mwakani hawezi kuweka malengo ya ndoa kwani bado kuna mambo yake hajayaweka sawa hivyo suala la kuolewa ataliweka hadharani baada ya miaka miwili ijayo.

“Sina mpango hata kidogo kwa mwaka huu wala mwakani labda baada ya hii miaka kupita ndiyo ninaweza kupanga tena suala la ndoa,” alisema Lulu.


Hata hivyo, alipotakiwa kumtaja mpenzi aliyenaye kwa sasa, Lulu aligoma kumtaja lakini akakubali kuanika siri za mwanaume anayetaka kuwa mumewe.

“Kwanza nahitaji mwanaume atakayenielewa kwa kila kitu, pia awe na mapenzi ya kweli na atakayeniangalia kama Lulu na siyo kama Elizabeth pekee. Anapaswa kutambua na kusapoti kazi zangu za sanaa,” alisema Lulu.

Mbali na hayo pia Lulu alielezea mikakati yake ya sanaa mwaka huu, ambapo alisema ana mpango wa kuendelea na masomo huku akiwa pia na ‘project’ kubwa mbili ambazo anatarajia kuzifanya.


Nina project kubwa mbili mwaka huu, muda utakapofika kila mmoja atazijua maana nitaziweka wazi,” alisema Lulu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname