FAHAMU PISHI MAHUSUSI KWA WEEKEND HII



Mara nyingi siku za weekend hususani Jumapili watu wengi hutumia siku hii kutathimini kuhusiana na mambo mbalimbali ya kazini yaliyojiri wiki nzima pamoja na kujiandaa kuikabili wiki inayofuata, lakini kitu kizuri na muhimu zaidi ambacho ni vyema kukizingatia katika mapumziko ya weekend ni pamoja na kula chakula kizuri, hivyo basi kwa kulitambua hilo habarimkusanyiko.blogspot.com inakuletea namna ya kupika Maini ya kuku siku hii ya leo

MAHITAJI

Maini ya kuku nusu kilo

Mafuta ya kupikia

Vitunguu maji vikubwa 2

Limao moja/ mawili

Hoho 1

Chumvi

Pilipili 1

Kitunguu Swaum

Tangawizi 1 kijiko cha chai

Curry powder 1/2 kijiko cha chai

MATAYARISHO 
Safisha maini yako vizuri na uweka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu maji, swaum na tangawizi kwa pamoja, jitahidi vitunguu visiwe vya brown, kisha weka maini, curry powder, pilipili, chumvi, hoho na limao kisha changanya vizuri na ufunike.

Baada ya hapo pika mpaka maini yaive na hakikisha yanakuwa na rojo kidogo, kisha ipua na yatakuwa tayari kwa kuliwa na chochote upendacho kama vile chapati, chips, ugali, wali.n.k

Pishi hili limeandaliwa na kuletwa kwenu na Asha Habibu

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname