GESI CHAFUZI ZAELEZWA KUSABABISHA MAGONJWA YA MOYO NA MAPAFU
Makubaliano yamefikiwa huko barani Ulaya ya kuwezesha kupunguza utoaji wa gesi chafuzi zinazoweza kusababisha magonjwa hatari kwa binadamu ikiwemo moyo na mapafu.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mazungmzo yaliyoratibiwa na tume ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya, UNECE ambapo afisa wake Alisher Mamadzhanov, alisema kuwa gesi hizo chafuzi ni pamoja na Amonia inayopatikana wakati wa shughuli za kilimo mathalani kwenye mbolea ya samadi na ile inayotengenezwa viwandani.
Aidha, Alisher alisema kwamba gesi hizo zimekuwa zinasababisha chembechembe iitwayo PM2.5 ambayo ni hatari sana kwani inaweza kuingia kwenye mapafu na kuongeza kuwa chembechembe hizo zimetambuliwa na shirika la afya duniani (WHO) kuwa zinasababisha vifo vinavyoweza kuepukika.
Mbali na hayo, Alisher, alisema kuwa hivi sasa uchafuzi wa hewa kwa ujumla unaongoza kusababisha vifo Laki Sita kila mwaka kwenye ukanda wa Ulaya na vifo Milioni Saba kila mwaka duniani kote.
Sambamba na hayo makubaliano hayo yamepatia nchi za Ulaya mambo matano ya kuzingatia ikiwa ni kupunguza utoaji hewa chafuzi kwenye sekta ya kilimo ambayo inatajwa kusababisha asilimia 84 ya gesi ya Amonia iliyoingia hewani mwaka 2012 kwenye ukanda wa Ulaya.
Unastahili kupata habari zote kutoka kwetu kadri zinavyotufikia kila siku, asante kwa kuwa nasi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment