RAIS MUSEVENI AMEYATAKA MATAIFA YA AFRIKA KUJITOA ICC
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameyataka mataifa ya Afrika kujitoa katika mkataba unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, kwa kile alichodai kuwa taasisi hiyo ya kimataifa inawalenga waafrika isivyo haki.
Hayo aliyasema alipokuwa akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Kenya zilziofanyika mjini Nairobi, Rais Museveni amesema atawasilisha mswaada katika kikao kijacho cha Umoja wa Afrika ili mataifa yote wanachama yajiondoe katika mkataba huo wa ICC na kuwaachia magharibi wabakie humo.
Aidha, Museveni aliongeza kwamba yeye hapo awali alikuwa akiiunga mkono ICC kwa vile anaheshimu nidhamu na kutaka kila mmoja awajibishwe kwa makosa yake, lakini taasisi hiyo imegeuka ni chombo cha kuikandamiza afrika na kusema kwa maneno sitafanya kazi nao tena.
Itakumbukwa kwamba hivi karibuni waendesha mashtaka wa ICC hivi walimfutia mashtaka Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, lakini naibu wake bado anaendelea kukabiliwa na mashtaka katika mahakama hiyo.
Ni kila iitwapo leo huwa tunakuwa pamoja katika kuhabarishana, tafadhali endelea kuwa nasi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment