ALIYEMKEKETA MTOTO WA MIAKA 13 AFUNGWA MIAKA MIWILI JELA


Suala la ukeketaji limekuwa likifanyika sana katika nchi za Afrika kitendo ambacho kimekuwa kikigharimu maisha ya mabinti wengi na wanawake kwa ujumla kutokana na zoezi hilo kusababisha jeraha kubwa na kupelekea damu nyingi kuvuja.
Kutokana na kutambua madhara kama hayo huko nchini Misri daktari mmoja amejikuta katika mazingira magumu baada ya kuwekwa mbaroni kwa kosa la kumkeketa msichana mwenye umri wa miaka kumi na tatu.

Inaelezwa kuwa watetezi wanaopinga tabia hiyo ya kuwakeketa watoto wa kike nchini humo walishtuka baada ya Mahakama kumwachilia huru Daktari Raslan Fadl mnamo mwezi Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, baada ya kesi kusikilizwa upya daktari huyo amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka miwili gerezani.

Licha ya kuwepo kwa makatazo mbalimbali ya vitendo hivi vya ukeketaji wa wasichana miaka sita iliyopita nchini humo, lakini bado imeonekama zoezi hilo likiendelea kuwa kubwa.

Kufuata hukumu ya daktari huyo, wapambanaji wa masuala hayo ya ukeketaji nchini humo wameelezea hukumu hiyo kuwa ni ushindi mkubwa kwao.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname