KWA WEWE UNAYEPENDA KUPIKA TUUNGANE HAPA
Ikiwa leo ni Jumapili nzuri ya Disemba 26 mwezi wa Januari habarimkusanyiko.blogspot.com inapenda kukukaribisha 'Jikoni Kwetu' ili tuweze angalau kupika mwishoni mwa weekend hii.
Na leo tutakwenda kuangalia namna ya kupika pishi la la choroko na tunaanza namna hii Karibu!!
MAHITAJI
Choroko kikombe 1 na nusu
Nyanya 1/2 kopo
Swaum kijiko kimoja cha chai
Kitunguu kikubwa 1
Curry powder 1 kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Nazi kopo 1
Olive oil
Pilipili nzima
NAMNA YA MATAYARISHO
Unapotaka kupika pishi hili ni vizuri uwe umejipanga siku moja kabla maana ni vizuri ukaloweka choroko usiku mzima kisha siku inayofuata utazichemshe choroko zako hadi ziive kisha baada ya kuiva utaziweke pembeni.
Baada ya hatua hiyo utasaga nyanya zako na kuandaa kitunguu pamoja na swaum kisha utavipika mpaka kiasi, baada ya hapo tia mafuta na curry powder, pika mpaka nyanya zitoe mafuta kisha tia choroko, tui la nazi, maji nusu kikombe, pilipili na chumvi, kisha koroga vizuri na uache ichemke.
Pika mpaka tui la nazi litakapoiva na rojo ibakie kidogo sana, kisha ipua na mboga yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula mboga hii kwa wali, ugali na wakati mwingine hata kwa chapati inaenda pia. Asante.
Pishi hili maalum kwa ajili ya weekend yako limeandaliwa na kuletwa kwenu na Asha Habibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment