FAHAMU UZURI WA HIFADHI YA KISIWA CHA SAANANE




Tanzania ni nchi yetu ambayo imebarikiwa kuwa na vivutio vingi na tunapozungumzia vivutio hivyo ni pamoja na hifadhi za taifa zinazopatika hapa nchini.

Leo katika Jicho Letu Porini tunakuletea tunaanza hivi, miongoni mwa hifadhi za taifa ambazo hupatikana hapa nchini ni pamoja na hii Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane, hii ni hifadhi iliyoanzishwa kama bustani ya kwanza ya wanyama mnamo mwaka 1964. Lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa ni kuhamasisha uhifadhi na kuelimisha jamii.


Ni dhahiri kuwa wengi tunaweza tukawa tunajiuliza kuhusu jina la hifadhi hii na ni kwanini iliitwa Saanane, lakini ukweli ni kwamba jina la hifadhi hii lilitokana na mwanzilishi wa bustani aliyeitwa Saanane Chawandi. 

Kati ya mwaka 1964 na 1966 wanyama mbalimbali walihamishiwa katika kisiwa hiki, wanyama hao ni pamoja na mbogo, digidigi, tembo, pofu, pongo, swala pala, ngiri, pundamilia, twiga, nungunungu  n.k.

Na inaelezwa kuwa wale wanyama wakali kama faru na mbogo wao walikuwa wakifungiwa, na wale wanyama wapole waliachiwa huru, lakini baadaye bustani hii iligeuzwa kuwa pori la akiba (Game Reserve) mwaka 1991 na kupitishwa rasmi kuwa Hifadhi ilipofika mwezi Julai mwaka 2013. Ikiwa na eneo la mita za mraba 0.5, na iko umbali wa km 2 kusini magharibi kutoka katikati ya jiji la Mwanza katika Ghuba ya Ziwa Victoria.
Hii ni moja ya boti zinazotumika kupeleka wageni kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saa Nane.
Jinsi ya kufika katika hifadhi hii.
Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Saanane kinafikika kwa njia ya usafiri wa boti ukitokea Mwanza, Mtu anaweza kufika Mwanza kwa gari, ndege au treni na kutoka Mwanza mjini kwakutembea kwa miguu ama kwa gari hadi geti la kuingilia hifadhini.

Shughuli zinazofanyika hifadhini:
Hifadhi ya Kisiwa Cha Saanane inatoa fursa kwa mtalii kuja na kufanya shughuli mbalimbali anapokuwa ndani ya hifadhi pamoja na kuangalia wanyama, kukwea miamba, kutizama ndege, na safari za kutembea, vile vile kupiga makasia.

Mporipori wetu wa habarimkusanyiko blog anakujuza haya mengine kuhusu hifadhi hiyo. Je Wajua!
Hifadhi ya Saanane ni kisiwa chenye madhari mazuri kilichopo ndani ya Ziwa Victoria.

Pia kisiwa kipo karibu sana na jiji la Mwanza ni (Dakika 15 mwendo wa miguu)
Hali kadhalika hii ndio hifadhi ya mwisho kati ya hifadhi zipatikanazo nchini Tanzania, pia ndio hifadhi ndogo nchini Tanzania na Barani Afrika.

Kama ungependa kufika katika hifadhi hii tozo zipo hivi
Tozo katika hifadhi hii zimegawanyika katika makundi matatu, ikiwa na maana kuwa kundi la kwanza ni wale raia wa Afrika Mashariki, la pili ni kwa wageni ambao hutoka nje ya Afrika Mashariki yaani ambao si Wanaafrika Mashariki na kundi la tatu ni kwa wageni ambao sio Wanaafrika Mashariki, lakini wanafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki.

Age
East Africa Citizen
Non-East Africa Citizen
Expatriate
Below 5 years
Free
Free
Free
Between 5 and 16 years old
Tshs: 2,000/=
15 US $
5
16 years old and above
Tshs: 5,000/=
30 US $
15




Bush lunch (per head) excluding other fees
Tshs: 5,000/=
5 US $
5

Boat Charges
Trip
East Africa Citizen
Non-East Africa Citizen
Expatriate
Return trip for 20 pax
Tshs: 35,000
35 US $
35
Lake excursion 1 hr
161,000
100 US $
100
Lake excursion 30 minutes
80,500
50 US $
50

Other Fees:
Video recording in island: 100,000 for East Africa anda 100 $ for Non Citizen.
Video recording at office compound: 50,000 for East Africa anda 50 $ for non citizen.
Hiring of ground for special occasions at office Dock: 500,000
Note: All charges are subject to change any time.
 
USIKOSE KUTEMBELEA KISIWA KISICHOSAHAURIKA....JAMBO TANZANIA....!!!

Makala haya ya Jicho Letu Porini huandaliwa na Shadrack D. Daniel, na hutoka kupitia blog hii kila wiki siku ya Ijumaa, lakini endapo unafikiri ni wapi utapa gari zenye ubora kwa ajili ya kukodi basi mtafute Shadrack D. Daniel kutoka Kampuni ya Sam's Car Rental Tours & Safar's Ltd kwa simu namba 0654 022 054 au 0715 437 283 website ni www,samscarental.com.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname