SIASA:KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KIONGOZI ATOA AHADI KEM KEM KWA VIJANA
Makamu wa Rais wa chama cha wafanyabiashara wa viwanda na kilimo Taifa (TCCIA) ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa (CCM) Joseph Kahungwa, amewataka wananchi wa jimbo la Nyamagana jijini Mwanza kumpa ushirikiano katika uchaguzi ujao ili aweze kupata fursa ya kuwatumikia.
Hayo aliyasema juzi alipokuwa akizungumza na mwandishi wa blog hii, ambapo alisema kuwa amepata msukumo wa kugombea katika jimbo hilo kutokana na changamoto ya kiuchumi iliyopo.
“Watu wa Mwanza wanachangamoto nyingi hasa ya kiuchumi kwa kutokana na vijana kutokuwa na ajira na wanapotaka kujikwamua kufanya umachinga wanakosa maeneo hali inayosababisha kuporomoka kwa uchumi” alieleza Kahungwa.
Pia Kahungwa alisema, atawahamasisha vijana kujiunga katika vikundi mbalimbali vya uzalishaji na kuhakikisha wanakuwa na anuani inayojulikana ili kujua wanapatikana wapi ili tuweze kuwaunganisha na taasisi za kifedha kwa lengo la kuwasaidia kupata mikopo.
“Nitasimamia hasa tatizo la uchumi na kutafuta suluhu la haraka kwa vijana ili waweze kujiajiri wenyewe kwani wengi wao wamehitimu vyuo ila hawana kazi na huishia mitaani wakihangaika” alisema Kahungwa.
Mbali na hayo, Kahungwa aliendelea kueleza kutokana na nia ya dhati aliyonayo, mwaka 2010 aligombea, lakini kura hazikutosha na aliendelea kupambana na changamoto za wananyamagana katika kuzitatua ili kupata suluhu.
Hata hivyo, Kahungwa kitaaluma ni mtaalam wa maswala ya biashara na uhasibu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kati ya mwaka 1991 na 2005 kwa kiwango cha shahada ya udhamili.
Habari hii imeandikwa na Goodluck Ngowi ambaye ni mwanahabari wa habarimkusanyiko.blogspot.com anayewakilisha jijini Mwanza, endelea kuwa karibu nasi tukupe story zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment