STORY KUTOKA JIJINI MWANZA KUHUSU SEKTA YA UTALII
Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori kilichopo Pasiansi jijini Mwanza kimelalamikia ulegevu wa sheria za kuwabana majangili kwa madai kuwa hazikidhi vigezo.
Akitoa changamoto hiyo hapo jana mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, Mkuu wa kikosi cha ujangili kanda ya ziwa Benjamini Kijika, alisema sheri hiyo inakatisha tama kutokana na hukumu inayotolewa na mahakama kulingana na sheria hiyo.
Aidha, Kijika alisema sheria hiyo inaelekeza jangili kufungwa miaka miwili endapo atabainika kuwa na kosa ikiwemo na faini ya Shilingi milioni 10.
“Kikosi hiki kipo kwa ajili ya kuzuia ujangili pamoja na kusimamia kesi mahakamni, lakini tumekuwa na changamoto ya sheria kwa kweli hawa wenzetu watusaidie juu ya hukumu hizi, lakini pia tunaendelea kutoa mafunzo ya kupambana na ujangili uliokithiri,” alisema Kijika.
Aliendelea kuongeza kuwa kwa mwaka jana walifanikiwa kukamata majangili 33, kesi sita na kwamba tano bado zinaendelea kusikilizwa, huku moja ikiwa tayari imetolewa maamuzi.
Akichangia juu ya sheria hiyo Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Chuo hicho Renatus Mkunde, alisema kinachotakiwa mahakamani ni ushahidi, lakini kwa bahati mbaya kesi za ujangili mara nyingi zinakuwa hazina walioona tukio wakati wa usomaji wa kesi.
“Aliyeona tukio ni askari anayekuwa porini, kesi taarifa anapewa mtu mwingine, na kesi anasimamia mtu mwingine kwa maana hiyo basi unatakuta, lazima mahakama ichukue maamuzi kulingana na sheria iliyopo kwa sababu aliyepeleka kesi ameshindwa kujitetea na kumpa nafasi mtuhumiwa kujitetea” aliongeza Mkunde.
Habari imeandaliwa na kuandikwa na Goodluck Ngowi, mwandishi wa habarimkusanyiko.blogspot.com anayewakilisha jijini Mwanza, Asante kwa kutembelea blog hii ndugu msomaji wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment