IFAHAMU NCHI AMBAYO INATHAMINI LUGHA YAO YA TAIFA KIASI CHA KUPIGA MARUFUKA LUGHA NYINGINE NCHINI KWAO
Lugha ni moja ya utambulisho wa utaifa wa taifa lolote tukiacha vile viashiria vingine kama nembo ya taifa, watu n.k , hivyo kwa kulitambua hilo ni vizuri kuzingatia kuithamini lugha kwani ni moja ya utambulisho mzuri kwa taifa lolote lile ulimwenguni.
Kutokana na hili suala la umuhimu wa lugha, huko nchini Somalia Rais wa nchi hiyo amepiga marufuku ya matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za serikali na kusema kuwa lugha pekee ya mawasiliano katika ofisi hizo ni kisomali tu.
Raisi Hassan Shaykh Mahmud, aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 42 tangu kuanza kutumika kwa lugha ya Kisomali nchini humo, maadhimisho yaliyofanyika mjini Mogadishu kwa lengo la kutaka kuiimarisha lugha hiyo.
Rais huyo aliamuru matumizi ya lugha hiyo ya kisomali katika ofisi za serikali yaanze Januari mosi mwaka huu na kuendelea, huku akiagiza kwamba hata shughuli zote za kiserikali nchini humo ziendeshwa katika lugha ya kisomali na si lugha nyingine yoyote. Hali hiyo inasababisha lugha zote za kigeni kuwekwa kando na zitakuwa zikitumiwa wakati wageni kutoka nje ya somalia watakapo kuwa wakihudumiwa tu.
Naye spika wa bunge la Somalia, Muhammad Shaykh Usman Jawari, ambaye pia alitoa kauli yake kwenye maadhimisho hayo, na kusema kwamba ni jambo muhimu kwa jamii ya wasomali kuelewa umuhimu wa lugha yao na kuitaka jamii kuiimarisha lugha hiyo.
Source: BBC Swahili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment