Masuala ya urembo ni mambo ambayo yamekuwa yakipewa nafasi ya kwanza kwa mabinti wengi na wanawake katika mataifa mbalimbali, lakini Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Andressa Urach hivi karibuni amenukuliwa akisema “kupenda sana kujiweka urembo bandia nusura umletee mauti yake”
Taarifa zinasema kwamba Urach aliliambia jarida la Daily Mail la Uingereza kwamba alidungwa sindano za kemikali ili kufanya makalio yake kuwa makubwa pamoja na kuongeza ukubwa wa miguu yake. Lakini mnamo mwaka 2013, mwili wake ulianza kuoza ndani.
Taarifa zinaarifu kuwa athari za kujiweka urembo bandia zilianza kumwandama Urach hadi madaktari kulazimika kutoa kemikali hizo kutoka mwilini mwake mwezi Novemba kwa kuchimba mashimo katika mapaja yake.
Daktari mmoja wa kurekebisha na kutibu athari zinazotokana na urembo bandia alisema ugonjwa alioupuata Urach ulitokana na vifaa vichafu.
Hata hivyo, madaktari waliweza kuokoa maisha ya Urach, licha ya kuwa hadi leo anatumia tu kiti cha magurudumu na miguu yake ina mashimo mengi ambayo madaktari waliweza kutoboa wakati wakutoa kemikali zenye sumu alizotumia kuongeza ukubwa wa makalio na miguu.
''Ninalipia makosa yangu leo kwa sababu nilitaka urembo kwa kila hali, ili nionekane kuwa kamili. Mungu ananiadhibu'' Urach aliambia Mail.
Urach aliongeza kuwa ''lakini badala ya kujiongeza urembo, niliharibu mwili wangu na sasa hata hauna sura.'' Na kuongeza kuwa “Mungu alimpiga kiboko kwa kujaribu kujibadilisha mwili wake kwa sababu ya kujitakia umaarufu”
Urach pia alisema kwamba alikuwa na mazoea mabaya ya kufanyiwa uapasuaji wa kujiongeza urembo bandia kila alipojihisi kufanya hivyo.
''Sikuwahi kutafakari mara mbili wakati nilipokuwa nafanyiwa upasuaji, lakini watu waliponionya nilidhani tu nitaweza kukabiliana na athari za hayo baadaye na niliamini ningeweza kwenda kwa daktari, kama mfano nilivyozoea kwenda dukani na kuchagua nilichokitaka, pia nilitaka watu wanitazame na kusema tu, ''wow'' alisema Urach.
Urach akiwa hospitali baada ya kutolewa kemikali mwilini ( Tunaomba radhi kwa picha hii kutokana na kutozingatia maadili yetu ya Kitanzania) |
Urach akiwa hospitali |
Source: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment