IFAHAMU NCHI AMBAYO WAKAZI WAKE HAWANA HATA CHEMBE YA TABIA YA WIZI, KIASI KWAMBA UNAWEZA KUANGUSHA WALLET NA UKAREJESHEWA IKIWA SALAMA
IMEELEZWA kwamba Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee ya wakazi wake kuwa waaminifu baada ya kupimwa imani zao kwa kutumia pochi (wallet) iliyokuwa ikiangushwa mtaani.
Hayo yamedhihirika katika utafiti uliofanywa na mtengeneza filamu mwenye asili ya Uingereza alipokuwa katika mitaa ya Dubai na kujaribu mara arobaini na tano na kuidondosha kwa makusudi pochi (wallet) yake na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake.
Mtengeneza filamu huyo, Daniel Jarvis, mwenye miaka 26, alikuwa akifanya tukio hilo la kudondosha pochi yake hiyo, huku akiwa ameificha kamera yake na kurekodi mfululizo wa matukio hayo ya makusudi akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, huku lengo lao kubwa likiwa ni kutaka kujua uaminifu wa jamii hiyo. Na kuirushwa vipande vyake katika YouTube ambapo mpaka kufikia jana usiku watazamaji walikuwa ni zaidi ya 70,000.
Jarvis aliiambia 7DAYS walishangazwa na utafiti huo na kikubwa kilichowashangaza ni kwamba waliookota pochi hiyo hawakujishughulisha na kutazama ndani endapo kulikuwa na nini? Wakati pochi hiyo ilikuwa imesheni Euro za kutosha na fedha ya Falme za Kiarabu Dirham kadhaa.
Hata hivyo, Jarvis anasema mtaa wa kwanza walioufanyia majaribio ni mtaa uliko katika barabara ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates, lakini kila aliyeiona pochi hiyo aliirejesha, lakini anasema baadaye walifikiria labda sababu ya kurejeshwa pochi hiyo ilikuwa ni mtaa walioko kuwa ni eneo la watu matajiri.
Pamoja na kudhani hivyo, lakini Jarvis anasema pia utafiti wao waliuhamishia eneo la Bur, Dubai, mahali ambapo palionekana ni duni kidogo, lakini licha ya uduni wa mahali hapo cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyokuwa hapo awali, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Jarvis alisema pia walifanya utafiti kama huo katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu baada ya kuidondosha tu pochi aliyeiokota alianza kukimbia nayo, lakini pia huko nako hakukuwa na aliyethubutu kuichukua pochi hiyo.
Taarifa zinasema kwamba Jarvis, alivalia suti nadhifu na kuigiza kudondosha pochi, huku akionekana kwenye video hiyo anaeleza hisia za kurejeshewa kitu ulichodondosha kuwa ni raha iliyoje, lakini akaendelea kusema kuwa anadhani vyombo vya habari hupotosha ukweli, kwakuwa kulikuwa na kichwa cha habari kuwa kuna mtu alihukumiwa miaka 15 jela kwa kuiba mdoli wenye taswira ya dubu, utafiti wetu umegundua tofauti na wayasemayo.
Swali linakuja endapo mtafiti huyu Jarvis ataamua kufanya utafiti huu hapa nchini Tanzania pale maeneo ya Kariakoo mtaa wa Kongo, Je itakuwaje unaweza kutuambia unahisi ni nini kitatokea?
Source: BBC Swahili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment