WAFANYABIASHARA WAOMBA KUSHUKA KWA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI
Wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) na wafanya biashara wa soko la Kiloleli akatika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wamelalamikia gharama za usafirishaji kuendelea kuwa juu ingawaje gharama za mafuta zimepungua.
Malalamiko yao yamekuja siku chache baada ya Mamalaka ya Udhibiti wa bei za Mafuta nchini (EWURA) kutangaza kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo.
Akizungumza na blog hii jijini humo, Mwenyekiti wa soko hilo, Modest John, alisema wameendelea kupandishiwa bei za bidhaa na hakuna dalili ya kupungua kwa bei ya mafuta na gharama za usafirishaji kwa wajasiriamali wadogowadogo.
“Tangu EWURA watangaze sisi tunaona nauli ni zilezile, sio za mizigo au abiria, kwa hiyo kushuka kwa mafuta kwetu bado hakujatusaidia, hasa kwa watu wa chini tunaoanza,” alisema John.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Jasmine Selemani aliiomba serikali kusimamia punguzo la gharama za huduma za usafirishaji ili kuwapatia unafuu wa kimaisha. Huku akiiomba serikali kusaidia kuwarudisha machinga waliosalia maeneno ya mjini ili waendeleze shughuli zao katika soko hilo,
“Soko letu bado ni la kijijini, halina mvuto wa soko, sasa hivi watu wengi wanaishia mjini na masoko ya huko pembeni, sisi huku tunaendelea kutaabika,” alisema Selemani.
Meneja wa Mamalaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Bahati Musiba, alipoulizwa juu ya suala hilo, alisema hayuko tayari kulizungumzia kwani makao makuu walishalizungumzia.
Habari hii imeandaliwa na Goodluck Ngowi ambaye ni mwandishi wa blog hii kwa upande wa jijini Mwanza. Asante kwa kuendelea kuwa nasi msomaji wetu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment