TCRA YAFUNGA VITUO VYA TV NA REDIO KWA MAKOSA YA KUKWEPA KODI

Mamlaka ya Mawasiliano TCRA imevifungia vituo 21 vya Radio na 6 vya TV kikiwemo kituo chaStar TV, Radio free Afrika, Kiss Fm na Uhuru FM kwa kushindwa kulipa kodi ya lesseni kwa wakati .

Akitangaza uamuzi huo, mkurugenzi wa habari na mawasiliano wa TCRA Innocent Mungy, amesema kuwa mitambo ya vituo hivyo itazimwa ifikapo kesho Januari 17 saa 6 usiku, na itawashwa baada ya vituo hivyo kulipa madeni yanayowakabili na endapo kituo chochote kitakaidi basi kitachukuliwa hatua kali za sheria.

Mungi amesema endapo kituo chochote kitakacholipa ndani ya miezi mitatu kwenye kifungo hicho kitafungiliwa.

“Katika kipindi cha miezi mitatu kituo chochote kikilipa ada ya resini ,na akatimiza matakwa yote ya kisheria na akalipa pesa zote anazodaiwa basi sisi tutamfungulia”amesema Mungi,

Vilevile Mungi amedai kuwa endapo miezi mitatu ya kifungo hicho ikipita na vituo hivyo vitashindwa kulipa ada ya reseni basi Mamlaka hiyo itavinyang’anya reseni ya utangazaji na kuamuliwa kuanza upya kuomba reseni

Pamoja na hayo, Mungy amesema mamlaka hiyo haiwezi kusema ni kiasi gani cha pesa ambacho vituo hivyo vinadaiwa kwa madai kuwa kanuni na taratibu haziwaruhusu kutaja kiasi hicho kwa kuwa ni siri kati ya TCRA na mteja.

Mungy ameongeza kuwa TCRA imewataka wadau wote wa mawasiliano nchini kutii sheria bila shuruti na kufuata taratibu, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo la kuwasaka wanaokwepa kodi ni endelevu.

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname