Jambo hilo limezua mjadala kutokana na baadhi ya watu kusema kwamba ni haki ya kimsingi kwa mtu mwenye akili taahira kufurahia tendo la kujamiana na hata kuzaa, huku wengine wakisema kuwa watu hao hawawezi kujitunza wenyewe wala hawana ufahamu wa kuamua kilicho bora hivyo wasiruhusiwe kujitwika mzigo wa ziada.
Aidha, daktari bingwa wa maradhi ya akili katika hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Moi, mjini Eldoret, Edith Kwoba, alisema kuwa utafiti uliofanywa nchini Kenya unathibitisha kuwa asilimia 25 ya watu milioni 40 walioko nchini Kenya wana maradhi ya akili ingawa wengi wao hawajui, huku naye akiunga mkono kuwasimamisha uzazi wagonjwa wa akili:
Naye, mwalimu wa watoto wenye ulemavu wa akili, Mwalimu Mkuu wa shule ya mtakatifu Vincent De Paul katika eneo la Likuyani, kaunti ya Kakamega, Bw Konyango John Paul, alisema haki za kimsingi za watoto wenye akili taahira lazima zilindwe:
Mbali na hayo inaelezwa kuwa sheria nchini Kenya hazielezi kikamilifu iwapo wagonjwa wanapaswa kufungwa vizazi, huku kwa sasa kukiwa na kundi la kina mama walio na virusi vya HIV ambao wamefika mahakamani kuwashtaki baadhi ya madaktari kwa kuwafunga kizazi bila kuwafahamisha miaka ya 80.
Tunahakikisha hupitwi na story yoyote kila unapokuwa na habarimkusanyiko.blogspot.co tafadhali endelea kuwa nasi kila iitwapo leo
No comments:
Post a Comment