LAWAMA ZA WANANCHI ZAPELEKEA RAIS KUSHINDWA KUJIONGEZEA MSHAHARA


Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wamesitisha kujiongezea nyongeza ya mishahara yao baada ya kuibuka kwa malalamiko.

Taarifa zinaeleza kuwa nyongeza hiyo ilitarajiwa kuwa kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi, imesababisha kuzuka kwa malalamiko nchini Malawi, ambapo pato la nusu ya wananchi halifikii dola moja kwa siku.
Aidha, Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatajiongezea nyongeza hiyo ya mishahara hadi uchumi wa nchi hiyo utakapo tengemaa.

Itakumbukwa kwamba, kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150 milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusiana na masuala ya rushwa.

Mbali na hayo taarifa zinaarifu kuwa mishahara ya wabunge itazidishwa kwa asili 300%

Ni haki yako kupata taarifa zote kupitia habarimkusanyiko.blogspot.com, tafadhali endelea kuungana nasi kwa habari zaidi


No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname