RAIS WA SIERRA LEONE AAGIZA WAGONJWA WA EBOLA KUSAKWA NYUMBA KWA NYUMBA


Rais Ernest Bai Koroma

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ameamuru kufanyika kwa msako wa nyumba kwa nyumba kwa waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

Rais Koroma amesema kuwa, msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa Ebola.

Katika hotuba yake kupitia televisheni ya taifa, Rais Koroma amesema kwamba usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine ni marufuku pamoja na kufanya biashara siku ya Jumapili pia ni marufuku.

Mbali na kufutilia mbali biashara za siku ya Jumapili, imeelezwa kuwa mikakati hiyo mipya itashirikisha mda wa kununua bidhaa siku ya Jumamosi na katikati ya wiki.

Wataalam wa afya wakiwa katika mitaa ya nchi ya Sierra Leone
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO), Sierra Leone ni Taifa ambalo limeonekana kuathirika kwa sehemu kubwa na Ebola ambapo zaidi ya visa elfu nane vimeripotiwa kutokea nchini humo, huku mji wa Freetown ukiwa na rekodi zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi ya ugonjwa wa ebola katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.

Pamoja na kutolewa kwa makatazo ya kukusanyika kwa makundi ya watu, lakini taarifa zinaarifu kuwa wakaazi wa mji wa Freetown wamendelea kujumuika katika barabara mbali na kufanya mazoezi kwa pamoja licha ya tishio hilo la Ebola.

Itakumbukwa kuwa juma moja lililopita, wakuu wa nchi hiyo walifutilia mbali mikutano yote na sherehe za siku kuu ya Krismasi na mwaka mpya kama njia ya kukabiliana na kusambaa zaidi kwa Ebola.

Ni haki yako kupata habari zote kutoka kwetu, rafadhali endelea kutembelea habarimkusanyiko.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname