FAHAMU NAMNA YA KUISHI NA FURAHA MAISHANI MWAKO


Furaha ni moja ya suala muhimu sana kwa kila mwanadamu hapa duniani na ni wazi kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakiishi siku zote pasipo kuwa na furaha ndani ya kipindi cha muda mrefu.


Wengi wetu kuna wakati huwa tunajikuta tukikabiliwa na mambo magumu ambayo mara nyingine hupelekea hata kukata tamaa kabisa katika maisha yetu, hivyo kujikuta tukiishi pasipo kuwa na furaha kabisa.

Wataalam wa mambo ya saikolojia wanasema tatizo hili huweza kutatulika kwa kuanza na mhusika mwenyewe kulikubali tatizo hilo na kisha kuanza kulifanyia kazi.

Furaha hutegemea sana na wewe mwenyewe kuliko vitu au watu wengine, lakini hivi sasa kuna baadhi ya watu wanapitia katika hali ngumu ya maisha hadi kufikia hatua ya kushindwa kucheka au kufurahi, lakini hayo yote ni mambo yanayoweza kuchangiwa na wewe mwenywe pamoja na nafsi yako.

Moja ya mambo yatakayokusaidia kuwa na furaha ni pamoja na kuwa na moyo wa msamaha kwa wale wanokukosea. Inawezekana kuna mtu amekutenda kitu kibaya huenda kwa makusudi au bahati mbaya, lakini kwa ujumla wake tunasema amekukosea, tambua kwamba si vizuri kukaa au kuishi na kisirani kwa sababu ya mtu au watu waliokufanyia ubaya kwa muda mrefu hivyo ni vizuri kuwa na tabia ya kuyasahau maudhi unayoyapata kwa watu na inapobidi waelewe juu ya makosa yao kuliko kukaa na kisirani.

Pia ni vizuri kupenda kuamua kuwa mshindi katika maisha yako, jiamini kwamba wewe unaweza na ni mshindi pia hata kama unapitia mambo magumu kiasi gani, Hakikisha siku zote unachagua kufanya mambo yako kwa uhodari na kujiamini, hata kama baadhi ya watu watakuvunja moyo au kukudharau.

Mbali na hayo pia jitahidi kuwakwepa wale wanaochangia kuondoa furaha yako, hii ni kwa sababu inawezekana kila siku huwa upo karibu na watu ambao kwa namna moja au nyingine huchangia katika kuondoa furaha yako na huenda umekuwa ukijaribu kuwavumilia na kujikuta unashindwa kabisa basi kama ni hivyo ni vyema ukawapuuza au kama inawezekana kaa nao mbali.

Uadilifu na ukweli ni muhimu katika kukufanya kuwa na furaha hii ni kwa sababu kama wewe hupendi kufanyiwa hivyo basi na wewe usifanye kwa mwingine. Mtu unapokuwa muadilifu matokeo yake watu hukuamini katika mambo mbalimbali jambo ambalo husaidia kuimarisha furaha ya maisha yako zaidi pia.

Hayo ni baadhi ya mambo muhumu ambayo yanaweza kukusaidi kuwa mwenye furaha katika maisha yako.

MSOMAJI WETU TUNAPENDA KUKUKARIBISHA KUTANGAZA NASI SASA KWA GHARAMA NAFUU SANA,TUTAFUTE KWA SIMU NAMBA 0716 514 718/ 0656 268 623 AU EMAIL mkusanyikowahabari@gmail.com, KARIBU SANA

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname