ULE USEMI WA WANAUME NI WENGI KULIO WANAWAKE UMEDHIHILIKA BAADA YA MWANAMKE MMOJA KUAMUA KUJIOA MWENYEWE


Huwa kuna ule usemi kuwa kuolewa eti ni bahati na Mungu ndiye pekee anayepanga, lakini pia wengine husema eti hapa ulimwenguni wanaume ni wengi kuliko wanawake, inawezekana misemo hiyo ikaanza kuwa na ukweli wake kwa mbali hii ni baada ya mwanamke mmoja kukosa bahati hiyo ya kuolewa na kuamua kujioa yeye mwenyewe.
Inaelezwa kwamba, mwanamama huyo Yasmin Eleby akiwa na umri wa miaka 40 pasipo kupata bahati yoyote ya mwanaume aliyetaka kumuoa na hivyo akaamua kufanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, ambapo aliamua kujioa mwenyewe.

Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com, Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.

Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo alifanya harusi yake mwenyewe katika makazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa, huku sherehe hiyo ikiendeshwa na dada yake hii ni kwa sababu ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe, kwani harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.

Yasmini Eleby ndani ya siku ya harusi yake ya kujioa yeye mwenyewe
Aidha, baadhi ya majirani wa Eleby walisema hawaoni vibaya kwa Eleby kuamua maamuzi hayo na hiyo inaonesha Eleby anajikubali na anaamini kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.

"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' alisema mmoja wa majirani aliyeitwa Guess Jr .

Mbali na hayo jirani huyo alisema anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani kwani ni mrembo na anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani.
NDUGU MSOMAJI WETU ANZA SASA KUTANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU SANA KUPITIA BLOG HII, WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0656 268 623/ 0716 514 718 AU EMAL mkusanyikowahabari@gmail.com. KARIBU SANA!!

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname