VIONGOZI WA KIDUNIA WAAMUA KUOKOA MAISHA YA WATOTO KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA


Watoto wanaofariki kutokana na maradhi yanayoweza kuepukwa, kama vile surua bado ni kubwa katika nchi zinazoendelea, lakini tatizo hilo huenda likafikia mwisho baada ya wafadhili wa kimataifa kukusudia kuibadilisha hali hiyo.
Waziri wa Ujerumani anaeshughulikia ushirikiano wa maendeleo Gerd Muller amesema hadi kufikia mwaka wa 2030, hakuna mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano atakayeachiwa afariki kutokana na maradhi yanayoweza kuepukwa.

Hayo yalisemwa na waziri huyo kwenye mkutano wa wafadhali wa kimataifa uliofanyika mjini Berlin, ambapo washiriki walijadili mikakati ya kutoa chanjo za kuyakinga maradhi kama surua, kifaduro, homa ya manjano na maradhi ya kupooza.

Mkutano huo unaofahamika kama mfungamano wa kimataifa wa chanjo dhidi ya maradhi yanayoweza kuepukwa (GAVI) uliwakutanisha pamoja viongozi, kutoka nchi zinazoendea ikiwamo Tanzania na wafadhili kutoka duniani kote.

Aidha, akihutubia kwenye mkutano huo wa "Gavi" Rais Jakaya Kikwete alibainisha juu ya mafanikio ya nchi katika kutoa chanjo kutokana na msaada wa ‘Gavi’ , ambapo alisema kutokana na msaada wa ‘Gavi,’ Tanzania imeweza kutoa chanjo mpya 11, huku akiongeza kwamba, Tanzania ni miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zinazotoa chanjo kwa mafanikio.

Rais Kikwete alisema asilimia 90 ya watoto hapa nchini Tanzania wamechanjwa ili kukingwa na maradhi ya kupooza na asimilia 90 nyingine wamepewa chanjo ya kuuzuia ugonjwa wa surua.

Mpango unaokusudiwa kutekelezwa na asasi ya Gavi ni kutoa chanjo kwa watoto Milioni 300 katika nchi zinazoendelea hadi mwaka wa 2020.

Gavi ni ushirikiano kati ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Benki ya Dunia, Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa na wafadhili kadhaa wa kimataifa ikiwa ni pamoja na Wakfu wa Bill Gates.

Kiasi cha fedha kinachohitajika ili kuweza kuendelea huduma ya chanjo ni Euro Bilioni 6.6, ambapo Wakfu wa Bill Gates umechangia kiasi cha dola Bilioni 1.5. Huku Gates akisema ndoto yake ni kuona kwamba kila mtoto anapata chanjo za kukinga maradhi, lakini pia Ujerumani itachangia kiasi cha Euro Milioni mia sita.
 NDUGU MSOMAJI WETU ANZA SASA KUTANGAZA NASI KWA GHARAMA NAFUU SANA KUPITIA BLOG HII, WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0656 268 623/ 0716 514 718 AU EMAL mkusanyikowahabari@gmail.com. KARIBU SANA!!

No comments:

Post a Comment

Ad Inside Post

Comments system

Disqus Shortname